Saturday, July 21, 2007

MKALI WA BONGO AMPACHIKA MIMBA MKALI WA KENYA!!!


Ama kweli wahenga hawaongopi, kwanini? Walisema mficha uchi hazai, unakumbuka jinsi Amani na AY walivyojitahidi kuzima uvumi wa wao kuwa na uhusiano wa kimapenzi? Walizani mapenzi yana siriii, sasa limebumbuluka Amani huyo ana mimba.


Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari (jina tunalihifadhi) ni kuwa mapenzi ya siri baina ya wasanii hao yamefikia kikomo baada ya Amani kuamua kushika mimba ya AY. Chanzo hicho kilidai kuwa licha ya mwanadada huyo kuwa na ujauzito wa AY bado wanataka iwe siri kubwa.


“Unajua jamaa (anamtaja) hapendi kuweka wazi mambo yake binafsi hata siku moja ndio maana siku zote amekuwa akikanusha taarifa za yeye kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Amani, sasa sijui akijifungua itakuwaje?” kilisema chanzo hicho. Mwandishi wetu alimpigia simu AY kutaka kujua kuwepo kwa ukweli wowote wa madai ya yeye kumpachika mimba Amani, lakini hakueleza chochote.

Kufuatia kukaa kwake kimya gazeti hili liliamua kumpigia rafiki yake wa karibu (jina tunalihifadhi) na kuthibitisha kuwa Amani ni mjamzito.


Risasi: Mkubwa mambo vipi?

Rafiki wa AY: Shwari mtuwangu

Risasi: Ebwana nasikia mshikaji wetu AY kafanya kweli kwa Amani.

Rafiki wa AY: Hiyo siyo habari mbona? Umehama mji nini? Amani ndio hivyo ana ‘kitu’ cha miezi kama minne hivi.

Risasi: Dah nilikuwa sijui mtuwangu

Rafiki wa AY: Ok, sorry kwani naongea na nani?

Risasi: Risasi linajitambulisha.

Rafiki wa AY: Mamaaaa, ndugu yangu usiende kuandika habari hizi tafadhali sana.

Risasi: Kwanini nisiandike kwani si jambo la kheri hilo ndugu yangu?.

Rafiki wa AY: Sawa lakini ni mambo yake binafsi! (anakata simu).

Risasi: Haloo!! Haloo!! (kimya)

Kwa upande mwingine gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Amani bila mafanikio.

1 comment:

Anonymous said...

Hawa wenye magazeti ya bongo hawana chochote cha maana wanachofanya zaidi ya udaku, fitna, majungu na unafiki.

Udaku: Hivi kwanini ufatilie maisha ya mtu binafsi maisha ambayo hata ukiwaambia wanajamii hayawasaidii, ni sawa na hili gazeti likasomwe na mtu wa kijijini kabisa utamueleza nini? au umesaidia nini? baada ya kugundua kuwa AY amemtia mimba Amani? tafuteni habari zina faida kwa wananchi wa mjini na vijijini na sio udaku tu usio na maana kukosesha watu amani watu wanakuwa hawana hata raha na maisha yao!!!

Fitna: Kutoa habari kama hiyo ni kama kumfitinisha Amani na wazazi wake kuwa yeye ana mimba na kuona ametia aibu, hapo mnakuwa mnagombanisha wazazi na watoto wao hamtumii hata akili bwana ovyooooooo.

Majungu na unafiki: Nakumbuka vyombo vya habari vilikuwa vinamuandika marehem Amina Chifupa (mungu amrehem) kwa vibaya na kwa vitu vya uongo, au vitu vya kumuadhirisha na kumumbua bila sababu yoyote, wakati kuna mema ambayo alifanya hatukuona mkiyaandika, leo ameshakufa ndo mnasifia huo ndo unafiki kwanini hizo sifa msipe tangu yuko hai hamna maana hata kidogo nyinyi waandishi wa magazeti ya udaku hivi nyie waandishi dada zenu wako sawa na shangazi zenu? mbona hamuwatoi kwenye magazeti?

Abdallah asante sana kwa blog yako ni bomba sana na ni nzuri kaka naamini hii ndo blog itakayoongoza na wengine watajikongoja tu.