Thursday, July 19, 2007

RAY C MGONGO HUOO!!


Mbunge mmoja machachari na mwenye msimamo mkali bungeni, ambaye ni kijana na hana mke, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuona 'mgongo' wa mwanadada Ray C katika gazeti dada, Ijumaa Wikienda ya wiki hii.

Tukio hili la aina yake lilitokea siku hiyo hiyo katika baa maarufu ya Chako ni Chako iliyopo Dodoma mjini ambayo wabunge wengi hukaa jioni baada ya vikao vyao ambako Mbunge huyo na mwenzake kutoka Chama cha Upinzani cha CUF ambaye pia ni kijana walikuwa wameketi wakinywa huku Mheshimiwa akisoma gazeti hilo.

Mwandishi wetu wa Dodoma aliyekuwa pembeni akipata chakula chake, alifanikiwa kuyanasa mazungumzo ya wabunge hao wawili wakiongelea picha hiyo ya Ray C. "Aiseee huyu mtoto anatisha, utafikiri Beyonce, hizo ndizo figa ambazo mimi huwa nazitaka, si unajua. Mpenzi wangu wa zamani alikuwa mnene, mimi hivi sasa nataka shepu kama hizi, lazima nimpate huyu Ray C hivi nikijifanya kumtafutia tripu ya nje kimuziki atakataa?"

Mbunge mwingine: "Sijui, labda ujaribu, tatizo lao hawa wanapenda wasanii wenzao, sisi wanatuona wazee, halafu ukiwa naye, anataka muwe kumbikumbi, kila mahali uende naye, wakati Shigongo naye yupo bize na magazeti yake!"

Mbunge: "Bwana nitajaribu bahati yangu hata kama ni mara moja tu inatosha, nitamtenngea fungu, hata posho zangu nitatoa!"

Kabla maongezi hayajaendelea, mhudumu alifika mezani na chakula, kilichoendelea baada ya hapo ni maongezi ya kawaida tena kwa sauti ya juu kuliko mwanzo. Kwa mwandishi wetu hii ilikuwa ni dokeza (tip) la habari, siku iliyofuata aliwasiliana na mwandishi Mariam Mndeme aliyeko jijini Dar es Salaam ambaye alimpigia msanii huyo anayeaminika kuwa ni mrembo namba moja nchini Ray C na kumpasha juu ya habari hiyo.

"Nimezoea kufuatwa na watu wa aina hiyo, kwa sasa nipo bize ndugu yangu, natafuta fedha na nimekua, kama kuna dili la shoo nipigie na siyo mambo ya wakware kama hao," alisema Ray C
Kwa hivi sasa Rehema Chalamila ndiye msanii wa Kitanzania anayeaminika kuwa na figa bomba kuliko wote.

No comments: