Thursday, July 19, 2007

KUDAADEKI WALAI!!!!



Na Mwandishi Wetu
Katika hali ya kustaajabisha dada mmoja aliyedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu kimoja nchini (jina tunalihifadhi) aliyetajwa kwa jina la Veronica Amos, amejikuta akifanyiwa kitu mbaya na vijana wa kihuni.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni usiku wa saa sita eneo la Ubungo, Maziwa jijini Dar-es-Salaam kwenye kichochoro kimoja cha mtaa, ambapo vijana hao walimvamia dada huyo 'sistaduu' na kumchania nguo kisha kumpora simu.

Shuhuda wetu aliyekuwepo eneo la tukio ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alidai kuwa, dada huyo alikuwa akitokea kuponda starehe ndipo alipopatwa na balaa hilo.

"Yule dada ni mwanafunzi wa chuo kikuu (anataja jina) mara kwa mara amekuwa akipita maeneo ya hapa nyumbani usiku, amepanga nyumba ya tano kutoka ninapoishi, siku hiyo alipita kama kawaida yake, nadhani alikuwa anatoka kustarehe.

"Usiku nikiwa nimejipumzisha nilisikia mtu akipiga kelele nikajua vibaka wanafanya kazi yao, lakini baadaye nikasikia sauti ya mwanamke anaita jina la Soud ambaye ni kijana wa mtaani kwetu, ikabidi nitoke nje, hatua chache nikamuona yule dada akiwa anagombaniwa na vijana wa kihuni huku tayari wakiwa wameshamchezea ‘rafu’.

"Wakati wanaendelea na zoezi lao nikawapiga picha (zilizotumika ukurasa wa mbele), walipoona mwanga wengine wakatimu mbio, wakabaki vijana wawili, wakataka kunivamia, lakini wakati huo watu walikuwa wameshafika wakanisaidia tukamuokoa yule binti, sasa sijui walikuwa na lengo la kumbaka au kumuibia, " alisema mtoa habari wetu huyo.

Aliongeza kuwa, walimpomuuliza yule msichana alisema kuwa alikuwa anatoka kujisomea kwa rafiki zake, jambo ambalo watu wengi walilipinga kutokana na ukweli kwamba binti huyo alikuwa amevaa vivazi vya ajabu huku akionekana kukolea kilevi, jambo lililoashiria kuwa alikuwa ametoka kujirusha.

Mnyetishaji huyo alizidi kudai kuwa, katika varangati hilo wahuni hao walifanikiwa kumpora dada huyo simu yake ya mkononi aina ya Nokia.

Aidha alielezwa kuwa, tukio hilo si la kwanza kutokea katika eneo hilo kwani wiki moja kabla kijana mmoja aliyekuwa amelewa chakari naye alivamiwa na vibaka hao ambao walimuibia simu pamoja na viatu vyake.

Hata hivyo, uchunguzi ambao umefanywa na Amani umebaini kuwa, katika maeneo ya mjini akinadada ambao hupenda kulewa chakari na kuchelewa kurudi majumbani kwao wamekuwa wakijikuta wakifanyia vitendo hivyo viovu bila matarajio yao.

Gazeti hili linawaomba wasichana kujiepusha na unywaji pombe kupindukia pamoja na kuvaa mavazi yasiyo ya heshima kwani kwa kufanya hivyo, wanajiweka katika mazingira mazuri ya kufanyiwa kama alivyofanyiwa mwanafunzi huyo-Mhariri.

No comments: