Wednesday, July 11, 2007

KANUMBA NA WEMA, RAY NA LISA.. mmh!!


(Tanzania - July 12, 2007)
Na Richard Manyota

Sanaa ya uigizaji filamu inayowaleta pamoja wasanii wa luninga na baadhi ya mamiss Tanzania, imetajwa kuwa ni moja kati ya mambo yanayotafsiri laivu hisia za mapenzi zilizopo kwa mastaa hao.

Steven Kanumba 'Kanumba' msanii mahiri wa maigizo nchini na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu (angalia picha yake kulia), wameigiza pamoja kama mtu na mpenzi wake katika filamu bomba ambayo bado iko jikoni, huku Vecent Kigosi 'Ray' na Miss Tanzania namba tatu 2006 Lisa Jensen (angalia picha yake kulia) wakionesha kuwa wapenzi ndani ya filamu ya Fake Pastors.

Hata hivyo umahiri wa uigizaji wao ndani ya filamu hizo, umewafanya baadhi ya watu kwenda ndani zaidi na kusema kuwa, huenda kuna chembe za ukweli ndani ya uigizaji wao kama wapenzi.

"Niliona baadhi ya sehemu ya filamu ya Fake Pastors, kusema kweli sijapata kuona, ni nzuri na inavutia sana, ila nashindwa kuamini kama Ray na Lisa walikuwa wanaigiza tu.

"Nilishindwa kabisa kutofautisha uigizaji wao na tukio la live, yaani kama kweli wanaigiza basi wamefanya kitu cha kushangaza na kufurahisha sana, waigizaji wetu watakuwa wamepiga hatua," alisema mama Fredy mkazi wa Msasani jijini Dar es Salaam.

Aidha kufuatia msisimko wa filamu ya Fake Pastors uliozagaa mitaani na uvumi wa Ray na Lisa 'kubonyezana kizenji' mwandishi wetu alikutana na msanii huyo na kumuuliza ukweli wa mambo, ambapo ufafanuzi wake ulikuwa hivi:

"Sio kweli kama mimi na Lisa ni wapenzi, kinachoonekana katika filamu ni umahiri wa uigizaji wetu tu, tumefanya hivyo ili kurekodi picha katika kiwango cha kimataifa, nadhani unaziona," alisema Ray huku akionesha picha ambazo zimetumika katika ukurasa wa mbele wa gazeti hili.

Aliendelea kusema kuwa, uigizaji unahitaji uwezo wa kutafsiri matukio ya kutunga kuwa ya kweli hasa pale yanapotazamwa, kama inavyofanyika katika nchi zilizoendelea.

Aidha Ray alimsifu mnyange huyo kwa umahiri aliouonesha katika kuigiza, ambapo pia alisema Fake Pastors ni filamu nzuri iliyosheheni mafundisho lukuki, ambapo maelezo zaidi kuhusu filamu hiyo yapo ukurasa wa sita.

Katika hatua nyingine Kanumba na Wema wamekuwa wakihusishwa moja kwa moja na uhusiano wa kimapenzi kutokana na nyendo zao, hata hivyo Amani limeshindwa kukutana na mastaa hao ili nao waweke wazi uvumi huo ulionea mitaani.



KAKOBE KUJENGEWA HAKALU LA BILIONI 1.4!

Na Mwandishi Wetu
Kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa nyumba ya kifahari (hekalu) ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (F.G.B.F), Zacharia Kakobe, kufuatia michango iliyotolewa na waumini wake, Amani limeelezwa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, uchangishaji huo kwa ajili ya zoezi hilo umekuja kufuatia ombi la kiongozi huyo kutaka waumini wamnunulie gari kutokana na lile alilokuwa akitumia kuchakaa.

Ilielezwa kuwa, kufuatia ombi la Kakobe, waumini hao wakishirikiana na wafanyabiashara mbalimbali waliowahi kufanyiwa miujiza ya kiroho na kiongozi huyo waliamua kuchanga fedha kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.

Aidha chanzo hicho kimezidi kufafanua kuwa, waumini hao licha ya ombi la kiongozi wao kutaka anunuliwe gari pia waliona ni vema kumjengea nyumba ambayo itaendana na hadhi aliyonayo.
"Licha ya yeye kuomba kusaidiwa kununuliwa gari, waumini pamoja na wafanyabiashara mbalimbali wa Dar es Salaam na mikoani waliahidi kuchangia kwa ajili ya kumjengea nyumba ya heshima kufuatia ile ya Kijitonyama, Dar es Salaam, kutokuwa na hadhi," kilidai chanzo hicho.

Chanzo hicho cha habari kilizidi kueleza kuwa, waumini hao wamedhamiria pia kuwanunuliwa magari watoto wa kiongozi huyo kwa ajili ya kutembelea.

Habari zinadai kuwa, katika kufanikisha zoezi hilo, maaskofu wa mikoa mbalimbali nchini walikutana mkoani Dodoma mwanzoni mwa wiki iliyopita kufanya tathmini ya michango hiyo ambapo ilibainika kuwa kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kilikuwa kimeshakusanywa.

Wakizungumza na Amani kwa masharti ya hifadhi ya majina yao, baadhi ya maskofu hao wamethibitisha kufanyika kwa michango hiyo na kueleza kuwa, lengo hasa ni kuhakikisha kiongozi wao anakuwa na maisha mazuri.

"Tuliguswa sana pale makazi ya kiongozi wetu yalipooneshwa kwenye televisheni moja na kuona kwamba anaishi kwenye nyumba isiyorandana na heshima aliyonayo katika jamii.

"Ukichukulia kwamba, viongozi wanaweza kumtembelea nyumbani kwake ikawa aibu, ndio maana tumeamua kuendesha zoezi hilo," alisema mmoja wa maaskofu hao.

Amani lilifanya jitihada za kumtafuta Askofu Kakobe ili kuzungumzia zoezi hilo lakini hakuweza kupatikana mara moja. Hata hivyo, wakati kiongozi huyo akichangiwa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo uchunguzi umebaini kuwa, baadhi yao hawana hali nzuri sana ya kimaisha.

Licha ya waumini hao kuwa katika hali hiyo, mapenzi ya dhati kwa kiongozi wao ndiyo yaliyowasukuma kutoa michango yao bila kulazimshwa. Kanisa F.G.B.F ni moja kati ya makanisa makubwa ya kiroho nchini Tanzania.

4 comments:

Anonymous said...

mmmh tena pesa wala hazilipiwi kodi ama kweli dini siku hizi ni biashara inayolipa.

Anonymous said...

Mtumishi wa Mungu anahitaji luxury zote hizo?

Anonymous said...

wema aka chawote akatai tid sasa kanumba badee mimi

Anonymous said...

ndio maana nimeamua kwenda nigeria kusomea huwo usani nami nije anzisha kanisa langu watu siwaoga tena wana fanya dini biashara