Sunday, July 15, 2007

RAY C TISHIO AFRIKA MASHARIKI!!!


  • Wakati Tuzo za Kisima zitolewazo nchini Kenya zikiwa zinafanyika Agosti mwaka huu, baadhi ya wakali wa muziki wa Bongo Flava wametajwa kuwemo ndani ya kinyang'anyiro hicho, akiwemo Rehema Chalamila 'Ray C', ambaye kazi yake ya Sogea Sogea imetajwa kuwania wimbo bora kwa upande wa wasanii kutoka Tanzania.

  • Hiyo inaonesha ni jinsi gani mwaka huu ulivyokuwa wa neema kwa binti huyo, kwani hivi karibuni alifanikiwa kukamua tuzo za James Dandu na kabla jua halijazama ametajwa tena kuwania tuzo hizo, ambazo zimetokea kujipatia umaarufu Afrika Mashariki na nchi nyingine za mbali.

  • Akipiga stori na Abby Cool & MC George Over The Weekend, 'Kiuno bila mfupa' alisema kwamba amefurahishwa na kitendo cha waandaaji wa Kisima kumpambanisha katika tuzo hizo. "Sijisifii kwa hilo, lakini uhakika wa kushinda upo" alitutonya Ray.

  • Mbali na Ray C, wasanii wengine kutoka Bongo waliotajwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na Ambwenye Yesaya 'A.Y' ambaye kupitia kazi yake, Usijaribu, anawania tuzo ya wimbo na video bora kutoka Tanzania, Seif Shaban anawania wimbo bora kupitia kazi yake, Vailet.

  • Wengine ni Abubakari Katwila 'Q-Chiller' ambaye anawania tuzo ya wimbo bora kupitia wimbo wake wa 'Ukimwi', huku kundi la 2Berry, ambalo hivi sasa halipo tena, kupitia kazi yao ya Na Wewe likitajwa kuwania video bora. Msanii mwingine anayewania video bora kutoka Tanzania ni Jaqueline Ntuyabaliwe 'K-Lyinn', kupitia wimbo wake Crazy Over You.

No comments: