Saturday, August 11, 2007

DENTI AFUMWA 'AKIKANDAMIZWA KIBARA' USIKU WA MNANE


Catherine Kassally na Mariam Mndeme waliokuwa Morogoro

Mwanafunzi wa darasa la tano wa shule moja ya Msingi, mkoani
Morogoro aliyefahamika kwa jina moja la Emmy, amefumwa akiwa na

jamaa mmoja ‘mtu mzima’ wakiponda raha na mambo mengine machafu.
Denti huyo alifumwa na waandishi wetu, saa nane usiku, Jumatano
wiki hii kwenye sherehe za wakulima Nane Nane, katika viwanja
vya Mwalimu Nyerere, mjini Morogoro.

Denti huyo akiwa anaonekana ‘kuunyaka mtindi’ alikuwa
amekubatiwa na jamaa huyo ambaye jina lake halikuweza
kupatikana mara moja mbele ya kadamnasi ya watu katika grosari
moja iliyomo uwanjani humo.

Binti huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 na 14,
ambaye haikufahamika shule aliyokuwa akisoma, alikuwa amepakatwa
na jamaa huyo huku wakibusiana.

Waandishi wetu pamoja na baadhi ya watu waliokwenda katika
viwanja hivyo, waliwashuhudia binti huyo na jamaa yake
anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35-40 jambo
lililowafanya wawashangae na kulaani kitendo hicho kichafu.

Hata hivyo, baada ya vitendo hivyo kuendelea kukithiri baadhi ya
watu waliokuwepo katika eneo hilo walianza kuwakemea kwa
kuwataka waondoke, vinginevyo wangewaitia polisi.

Licha ya tishio hilo, wawili hao waliendelea kufanya uchafu wao
huku wakidai kuwa wasingewafanya chochote kwani walikuwa katika
raha zao.

Hata hivyo, jamaa aliyekuwa na denti huyo naye alianza kufoka
akidai kuwa wanawaonea kwavile ni waswahili kwani wangekuwa
wazungu wagewaacha.

‘’Hata kama mtawaita polisi, hawawezi kutufanya kitu kwani nyie
ndio mnaotutazama, kama mnaona noma basi msituangalie,
wangefanya wazungu mngesemasema maneno hayo?,” Alihoji jamaa
huyo.

Aidha, watu hao walishangaa wakidai kuwa jamaa huyo ni kubwa
kiumri hivyo alikuwa akimuonea kwa kumrubuni binti huyo
kutokana na umri wake kuwa mdogo.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza binti naye alianza kutoa

maneno ya kuwashambulia watu hao na kudai kuwa wawaache kwani
jamaa aliyekuwa naye anammudu licha ya kuonekana mkubwa kuliko
yeye.

“Mwacheni mpenzi wangu mwenyewe ninammudu na wala si mkubwa
kwangu mimi namuona kama mtoto mwenzangu,” alisema denti huyo.
Baada ya kuona wapenzi hao wanaendelea kufanya uchafu huo,
waandishi wetu walipowapiga picha ambapo awali waliduwaa lakini
baadaye walishtuka na kuacha.

Waandishi wetu pamoja na watu wengine waliokuwepo hapo
walipowasogelea, jamaa alinyanyuka na kumwacha binti huyo
ambaye aliomba msamaha baada ya kuambiwa kuwa picha yake
ingechapishwa kwenye gazeti.

“Mnisamehe dada zangu, haya ni maisha yangu na ni siri yangu,
shuleni kwangu hawajui, wala nyumbani kwetu hawafahamu sasa
mkitoa picha hiyo nitapigwa hadi kuuawa, niko tayari kuwapeni
hata fedha” alisema msichana huyo huku akimwaga chozi.
Msichana huyo aliondoka baada ya kuona kuwa ombi lake
halisikilizwi na wanahabari hao.

Tumelazimika kuziba sura ya binti huyo kutokana na sababu za
kimaadili - Mhariri.

3 comments:

Anonymous said...

Naomba nipate jibu kutoka kwenu nyie nyie wahariri wa hilo gazeti.Hivi Tanzania hakuna sheria inayokataza watu wazima kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watoto wa umri wa chini ya miaka 18?Kama ipo,waandishi wenu walichukua hatua gani,kama watu wazima,kulifikisha suala hili mbele ya polisi ili huyo kijana achukuliwe hatua kali?Kumrubuni mtoto kwenye mapenzi sio kosa?Wanawake tupooo??

Anonymous said...

Ndugu hapo juu,wenzio hawa wanataka hizo habari kuuza magazeti tuu ,inasikitisha ,kama kawaida hatua waliyochukua ni kuandika hiyo stori na kujiingizia faidaaa.Eti mtoto kaomba msaa halafu ,hivi kweli mtoto wa darasa la tano na hilo libaba.Nyie wapiga picha waandishi wanawake mliishindwa kuita hata polisi .HAKO KABINTI KANAWEZA KAWA KANA NGOMA TAYARI INATISHA SAANA:

Anonymous said...

inasikitisha kuona watu tunaowaita waandishi wa habari WANAUZA habari za mtoto wa darasa la TANO kujipatia faida, bila ya wao kuchukua hatua za kimsingi kama kuita polisi.
sasa kama kaomba msamaha ndo mumuandike gazetini?? ....kama mmekusudia kumfunza, na nyie ni wafunzaji hamtafuti habari kwa nia ya pesa , mngemchukulia hatua za kisheria huyo baba na sie kumtoa gazetini.
its very dissapointing to see watu tunaowategemea tanzania ndio wa kwanza to exploit us for there own good. so sad