Monday, November 26, 2007

Pnc: Kitu kigumu kwangu wakati wa kutongoza, sijui kuongea na madem, nina aibu sana

Mchizi aliyeingia ndani ya kumi na nane ya safu hii ni Pankras Ndaki Charles a.k.a PNC aliyetokea Mkoani Mwanza maeneo ya Pasias na kuhamia Dar es Salaam kunako familia ya Tip Top Connection kwa ajili ya kutafuta maisha kupitia sanaa ya muziki wa Bongo Flava.

Akiwa na umri mdogo, huku jina lake likiwa tayari vichwani mwa watu wengi, PNC alikutana na maswali mapya kibao, yakiwemo ya kizushi. Hebu yacheki.

1. Tabia zipi ulizokuwa nazo utotoni ambazo wazazi wako walikuwa hawazipendi?

Nilikuwa napenda kula sana, kutembea ovyo, vilevile nilikuwa mchafu ile mbaya kwasababu nilikuwa sipendi kuoga, kitu ambacho kiliwakera zaidi wazee.

2. Msichana mwenye umbo gani anakuzingua zaidi?
Nazinguliwa na msichana yeyote mrembo anayejipenda, ila ninaye wangu ambaye tunapendana sana.

3. Umeshawahi kutoswa ama kuwatosa mademu mara ngapi?
Duh! Hiyo kali, binafsi sijawahi kutoswa, ila kutosa nimewahi japo siyo wengi sana.

4. Nani wa kwanza kumkimbilia ukipata tatizo?
Watu wote walionizunguka au walio karibu na mimi Abdul Bonge, Babu Talle, Mully au Tip Top Family.

5. Ustaa umewahi kukusababishia matatizo gani?
Nashukuru Mungu tangu nimejulikana sijawahi kupata tatizo lolote kubwa mpaka nikashindwa kulitatua.

6. Kitu gani kigumu kwako wakati wa kumtongoza msichana?
Kitu kigumu kwangu sijui kuongea na madem, nina aibu sana

7. Uliwahi kugombana mara ngapi?
Niligombana sana wakati mdogo, lakini tangu nimekuwa na kuanza kujitafutia mwenye sijawahi kugombana na mtu.

Mengine kuhusu mchizi ambaye katika game ya muziki wa Bongo Flava kupitia 'kategori' ya kizazi kipya alitoka zaidi na kazi yenye jina la 'Mbona' bado anaisimamia albamu yake ya kwanza ambayo ipo kwa wadosi kitambo ikifanya vizuri sokoni na kazi nyingine kama I Need U, Huzuni, Nalia na nyinge kibao.

No comments: