Monday, November 26, 2007

TAMASHA LA UKIMWI bado siku 6

Zikiwa zimesalia siku sita ili itimie Desemba Mosi, siku ya Ukimwi dunia, wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake wanaisubiri kwa hamu kubwa burudani itakayoshushwa na mastaa mbalimbali wa muziki nchini.

Waandaaji wa tamasha hilo ambao ni Kamati ya Umoja wa Vijana CCM 'inayodili' na mapambano dhidi ya Ukimwi, wanawaomba wakazi wa Kanda ya Ziwa watakaofurika katika Uwanja wa CCM Kirumba siku hiyo, wajitolee vitu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima ambao wazazi wao walifariki kwa Ukimwi.

'Tunaomba watu wenye nguo hata zilizotumika, madaftari, kalamu, chakula na vingine ambavyo wanahisi vinaweza kuwasaidia yatima hao, sisi tutashukuru na kuwafikishia popote walipo' ilisema sehemu ya taarifa ya waandaaji waliyoitoa kupitia safu hii.

Baadhi ya wasanii watakaopanda stejini siku hiyo ni pamoja na Fareed Kubanda 'Fid Q', Joseph Haule 'Profesa Jay', Hamis Baba 'H. Baba', Hardmad, Ambwene Yesaya 'AY', Flora Mbasha na wengine wengi. Mbali na shoo hiyo vijana watapata fulsa ya kupiga stori na wenzao kuhusiana na gonjwa la Ukimwi, huku kauli mbiu yake ikiwa ni 'Zuia Ukimwi, tunza ahadi'. Hiyo siyo siku ya kukosa mtu wangu, kumbuka kwamba hakuna kiingilio.

No comments: