
Kampuni za QSSP Group kupitia Kituo chake cha Televisheni cha C2C na LIRO Promotion ndiyo waandaaji wa shughuli hiyo nzito ambao waliyataja makundi yaliyofanikiwa kupenya na kuingia kunako fainali hizo ambayo ni Jahazi Modern Taarab (Wana wa Nakshi nakshi), Dar Modern Taarab (Watoto wa Kandoro, Wajukuu wa Makamba) East African Melody (Watoto wa mjini).
Meneja wa C2C, Bahati Singh alisema kwamba baada ya kutolewa kwa kundi la Zanzibar Stars kupitia mchuo uliokuwa unafanyika katika kituo hicho cha televisheni, mashabiki wanatakiwa waendelee kuyapigia kura makundi hayo matatu ili kuliwezesha moja kuibuka na ushindi siku hiyo ya fainali.

Mpambano huo unakujia chini ya wadhamini kibao, ikiwemo Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Amani, The Bongo Sun, Championi, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
No comments:
Post a Comment