Friday, June 6, 2008

IJUMAA SHOWBIZ!


Kelly naye kudondoka Bongo
Kwa mara nyingine tena Wabongo wengi watakuwa wakisubiri kwa hamu kubwa kumwona supastaa mwingine kutoka Marekani. Sasa ni zamu ya Kelly Rowland, ambaye atatia maguu nchini mapema mwezi huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kituo cha Televisheni cha MTV, Kelly yupo katika ziara ndefu akizunguka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kutimiza majukumu yake kama Balozi wa mfuko wa MTV Staying Alive Foundation.

Mwanamuziki huyo ambaye ni mtunzi na mkali wa kuimba staili ya R&B ni miongoni mwa warembo watatu waliokuwa wakiunda kundi maarufu la Destiny'S Child, kabla hawajaamua kila mmoja kutoka kivyake.

Ndani ya kundi hilo walikuwemo yeye, Beyonce Knowles na Michelle Williams. Kwa sasa Kelly amesimama vyema na albamu yake iliyotoka mwezi uliopita, ikiwa na jina la ‘Ms. Kelly’. Ngoma yake ambayo iko juu ni ile inayokwenda kwa jina la Pumb Like This iliyomshirikisha binti, mkali wa michano, Eve.

“Mbali na kukanyaga Bongo, Kelly pia atadondoka katika nchi nyingine za Afrika kama Afrika Kusini, Ghana, Msumbiji, Kenya, Angola na nyingine,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo ya MTV.

Bado haijafahamika kama msanii huyo atakapo kuwa nchini kama atapanda stejini na kufanya angalau ‘free style’ ama la.

MB Dog: Kuiga kunawapoteza wasanii kwenye game
Kutoka pande za ‘Mabaibo Hosteli’, Dar es Salaam, kijana MB Dog amesema na ShowBiz kwamba kuiga staili za watu wengine ndiyo kunawafanya baadhi ya wasanii wapotee ghafla kunako game ya muziki wa Bongo Flava, hasa kupitia kategori ya kizazi kipya, Amina Salim alicheki naye.

MB ambaye jina lake kamili ni Mohamedi Mbwana, mwenye asili ya Mkoa wa Tanga, alisema kwamba anashangazwa na wasanii wengi hasa wanaoibuka hivi karibuni kutokuja na ‘idea’ (mawazo) mapya badala yake ‘wanakandamizia’ staili za wasanii ambao tayari wameshatoka kitu ambacho kinakuwa kigumu kwa wao kusonga mbele.
“Mambo ya kuigana sio mazuri kabisa, ndiyo maana kazi nyingi hazikai hewani kwa kipindi kirefu, zinapotea mapema.

Kwa mfano staili ninayofanya mimi hivi sasa wasanii wengi wanaifanya, matokeo yake huwezi kuwatofautisha, hiyo inawafanya wasanii wapotee mapema na kushindwa kukamilisha malengo waliyojiwekea zaidi ya kupoteza muda wake,” alisema Dog.

Baada ya kujichomoa ndani ya familia ya Tip Top Connection, mchizi ameungana na vichwa viwili vinavyofanya kundi lenye jina la Yakuza Mobb na tayari yuko hewani na ngoma yake mpya, ‘Natamani’ ambayo inabamba ile mbaya ikiwemo video yake.

**************************************************************

1 comment:

Anonymous said...

jamaa mbaya huyu