Sunday, November 16, 2008

IJUMAA SHOWBIZ

Ngwea: dili alizoomba zimetiki, sasa anakamata mahela

Kutoka ndani ya familia ya Chamber Squard, ShowBiz imeambiwa, kwamba, kijana Albert Mangwea a.k.a Cow Boy tayari ameanza kukamata dili kupitia ngoma yake, ‘Nipe Dili’ ambayo sasa ni gumzo karibu Bongo nzima.

Akipiga stori na safu hii, Ngwea ambaye ni miongoni mwa wasanii waliofanya vyema kunako tamasha kubwa la Fiesta 2008 lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam alisema kwamba, kupitia ngoma hiyo amerudi upya kunako game ya muziki wa kizazi kipya huku akiwa anakamatia dili mbalimbali zikiwemo shoo.

“Nataka kuwaonesha mashabiki wangu kwamba, kimya cha muda kilichopita ilikuwa ni kwa ajili ya kujipanga, sasa ni ngoma juu ya ngoma, mbali na ‘Nipe Dili’ tayari nimeshaachia kazi nyingine kama Mida Mibovu, Singida Dodoma na kadhalika ambazo zinapatikana katika albamu yangu mpya, ‘Nge 2800’.

Aidha mchizi ambaye katika albamu hiyo amefanya kazi katika studio tofauti, alisema kwamba, video ya ‘Nipe Dili’ tayari imeshafanyika kupitia kampuni ya Visual Lab na muda wowote kuanzia sasa itakuwa hewani.

1 comment:

Anonymous said...

Seif Jamal inspiration is to succeed in his Design career and clothing line. He wants to pursue his dreams as an artist while having fun and meeting great people all over the world along the way. Seif wants to be the first Tanzanian hiphop Designer to hit the mainstream and put Tz people on the map for the world to know. With all his hard work Seif’s wants to be admired and respected world wide. He puts in Tgp Clothing line% into all of his work and strives to bring out the best quality of clothes for his fans. Seif’s main goal is to be a part of the biggest concert ever in Tanzania and East African for Charity Events and etc. May Allah continue to bless him, his family, fans, his beautiful chick as his success grows.