Nyerere atingisha Marekani
Katika kuonesha kwamba, Bongo hivi sasa inatambulika na kuheshimika karibu ulimwengu mzima, kutoka pande za Marekani, jina la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere limeendelea kutesa baada ya msanii mkali wa R&B kuibuka na kutumia jina hilo.
Namzungumzia kijana kutoka Milwaukee, nchini humo, Nyerere Davidson (pichani juu) mwenye umri wa miaka 22 hivi sasa ambaye ameamua kuliendeleza jina la muasisi huyo wa taifa letu kupitia game ya muziki, huku tayari akiwa anafanya vyema na ngoma kadhaa.
Akipiga stori na mtandao mmoja wa burudani, Nyerere alisema kwamba, jina hilo alipewa na wazazi wake ambao walivutiwa na sifa alizokuwa nazo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ambao walimtaja kuwa alikuwa ni Rais wa Tanzania na Afrika kwa ujumla kwani alikuwa na nguvu ya kuleta amani, upendo na kiongozi shupavu.
Aidha ‘dogo’ alisema kwamba, kitu kilichomfanya awe juu ghafla kupitia game ya muziki ni sauti yake ambayo ni ya asili na kwamba alikuwa akiupenda muziki tangu alipokuwa na umri wa miaka 6. “Huwa nafanya muziki laivu kitu ambacho kimenipatia mashabiki wengi,” alisema.
Mbali na hilo, mitandao mingi ya ‘intaneti’ imekua akimzungumzia kijana huyo kwamba ana uwezo mkubwa na anaweza kuleta mapinduzi katika fani hiyo kwa kuwa anao uwezo wa kufanya staili tofauti kama nyimbo za Injili, Esgue Soul, Pop na R&B huku akiwa anatumia sauti ya kisasa.
“Nyerere yupo kufanya muhuri wa alama katika ulimwengu huu wa muziki, alinza kuimba akiwa na umri wa miaka 6 tu, alianzia kwenye kwaya kanisa kisha akaja kwenye maonyesho ya watu wengi wenye vipaji, sasa amweza kujulikana karibu dunia nzima,” ulisema mtandao mmoja wa burudani.
Kwa kifupi muziki wake umeweza kuwavutia pia mastaa wengi waliyopo katika fani hiyo kama Chaka Khan, Carl Thomas, Donny Hathaway, Floetry, Brandy, Freddie Jackson, Toni Braxton na Tonex. Hiyo inadhihirisha kwamba, Nyerere hivi sasa yuko juu na kwamba atalifanya jina la Baba wa Taifa liendelee kutingisha Marekani na duniani kwa ujumla. Vipi kwa wasanii wa Bongo, kwenu ikoje? Imetafsiriwa na Imelda Mtema.
@****************************************************************@
Ashanti!
Kupitia ‘Ebwana Dah!’ Leo tunamcheki uhusiano wa Ashanti Douglas na mastaa wa kiume kama baadhi ya wasomaji walivyoomba.
Akiwa anafanya vyema kunako sanaa ya muziki wa R&B, Ashanti amewahi kujiachia na mastaa wa kiume watatu ambao ni Irv Gotti ambaye alianza naye tangu mwaka 2001, kisha akaja kwa Nelly aliyeanza ‘kujiramba’ naye tangu 2003 japo amekuwa akikanusha kuhusu hilo.
Hivi sasa binti anajiachia na mtu mzima Antonio Pierce, japo bado haijawekwa wazi kama ameachana na Nelly. Kwa leo ni hayo tu kuhusu Ashanti.
@*******************************************************@
NAKAAYA: Akerwa na shutuma nzito, aizungumzia ‘ndoa’ yake
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Nakaaya Abrahamu Sumari a.k Mama Politician, hivi karibuni ameonesha kukerwa na skendo inayomuandama kila kukicha ya kuvaa mavazi ya nusu uchi lakini akidai haimnyimi mbavu.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Nakaaya alisema hataacha kutinga mavazi hayo hata akiolelewa.
“Mimi nashangaa sana wanaosema mavazi yangu mafupi. Hii ni staili yangu ya uvaaji toka nikiwa mtoto, sitaiacha hata nikiolewa, kwani sina nidhamu ya uwoga,”alisema Nakaaya.
Nakaaya ni mion goni mwa wasanii wa kike nchini wanaofanya vizuri kwenye gemu la muziki wa Kizazi Kipya.
No comments:
Post a Comment