Blue
Prof Jay
Tamasha la Ukimwi 2008: Songea kaeni tayari kwa shoo
Kamati ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi ya Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) inawaletea bonge la tamasha ambalo litawashirikisha wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Joseph haule Prof. Jay’, Ruta Bushoke ‘Bushoke’, Herry Samir ‘Mr. Blue’ na wengine kibao, litakalopigwa Desemba 1, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
Mratibu wa shughuli hiyo, Dk. Ringo Moses alisema kwamba tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka katika mikoa tofauti, mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na maandalizi kuwa makubwa zaidi tofauti na miaka iliyopita.
“Tunataka kila mwaka liwe tofauti kwa kuongeza vitu vipya, mbali na wasanii hao wa muziki wa kizazi kipya pia tutakuwa na wasanii wengine wengi wakiwemo wa sanaa za maigizo na nyimbo za injili ambao mbali na kutoa burudani pia wataongea na maelfu ya vijana watakaofurika siku hiyo kuhusiana na gonjwa hatari la Ukimwi,”.
Aidha mtaribu huyo alisema kwamba, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’, Luteni Yusuph Makamba ndiyo amepewa heshima ya kuwa mgeni rasmi siku hiyo. Mbali na Makamba viongozi wengine wengi wa Serikani watakuwepo kwa ajili ya kuongea na wananchi wa Songea.
“Tunawaomba wananchi wa Songea, hasa vijana wajitokeze kwa wingi ndani ya Uwanja wa Maji Maji ili waweze kubadilishana mawazo na wasanii pamoja na viongozi mbalimbali wa kitaifa, hilo nadhani linawezekana kwasababu kiingilio ni bure,” alisema Dk. Ringo.
***************************************************88
Mshindi kutajwa wiki ijayo
Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mpambano wa kumtafuta Ijumaa King Of Hip Hop, wasomaji na mashabiki wengi wanashahuku ya kutaka kufahamu kati ya mastaa hawa watatu, Prof. Jay, Johmakini na Fid Q waliyoingia kwenye tatu bora nani ataibuka na ushindi.
Kauli kutoka kwa mratibu wa shindano hilo, Charles Mateso, mshindi atatangazwa wiki ijayo kupitia safu hii baada ya zoezi kubwa la kuhesabu kura kukamilika. Unafikiri ni nani atalamba U-King huo? Cheki na sisi wiki ijayo.
TMK Family: Kumpongeza Obama Kenya
Baada ya kukamilisha ziara katika Mikoa ya Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita kundi la muziki wa kizazi kipya, TMK Wanaume Family linatarajia kuungana na maelfu ya wananchi wa Kenya kunako tamasha kubwa la Kumpongeza Rais mteule wa Marekani, Barack Obama, Hawa Mkombozi anadondoka nayo.
Akipiga stori na safu hii, kiongozi wa kundi hilo Said Fella alitamka kwamba, tamasha hilo litafanyika Desemba 6, mwaka huu jijini Nairobi na kwamba wamepata dili hiyo baada ya kazi zao nyingi kufanya vyema karibu Afrika mashariki nzima.
“Sijafahamu vizuri tutakuwa na wasanii gani wengine, lakini tumeambiwa ni tamasha la kumpongeza Rais wa Marekani, Barack Obama ambalo litafanyika uwanjani. Ubora wa kazi zetu ndiyo umetufanya tupate mwaliko huo maalum,” alisema Fella.
Wakiwa katika Mikoa ya Kusini, TMK Family walifanikiwa kupiga shoo sehemu mbalimbali kama Newala, Masasi, Nachingwea, Liwale, Mtwara na Lindi ambako pia walitoa misaada kama chandalua, nepi za watoto na unga wa ulezi kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali ya Sokoine. Safu hii inatoa pongezi kwa kundi hilo, ni mfano wa kuigwa na wasanii wengine.

********************************************************8

No comments:
Post a Comment