Tamasha kubwa la Ukimwi leo
Tamasha kubwa la Ukimwi lililoandaliwa na Kamati ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi ya Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) linafanyika leo ndani ya Uwanja wa Maji Maji mjini Songea huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’, Luteni Yusuph Makamba.
Mratibu wa tamsha hilo, Dk. Ringo Moses alisema na safu hii kwamba maelfu ya wakazi wa Songea, hasa vijana watakaofurika katika tamasha hilo watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wasanii kibao wakiwemo Maunda Zorro, Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Ruta Bushoke ‘Bushoke’, Herry Samir ‘Mr. Blue’ na wengine kibao wakiwemo wa mjini humo.
“Hili litakuwa ni tamasha la tatu la Ukimwi tangu tulipoanza mwaka 2006, kadri siku zinavyozidi kwenda tunaboresha zaidi, mtu aliyekuwepo kwenye tamasha la kwanza lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club 2006, akija Songea atagundua mabadiliko makubwa, kwani tumeboresha karibu kila sekta,” alisema Dk. Ringo.
Aidha, mratibu huyo alisema kwamba mbali na kupiga shoo ya nguvu, wasanii hao na wadau wengine wanaojihusisha na masuala ya Ukimwi watatoa mada mbalimbali kuhusiana na gonjwa hilo hatari. “Tunawaomba wananchi wa Songea, hasa vijana wajitokeze kwa wingi ndani ya Uwanja wa Maji Maji ili waweze kubadilishana mawazo na wasanii pamoja na viongozi mbalimbali wa kitaifa, hilo nadhani linawezekana kwasababu kiingilio ni bure,” alisema Dk. Ringo.
***************************
Likizo Tyme: Shoo kubwa wiki hiiIle shoo kubwa ya Likizo Tyme iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wapenda burudani nchini itaangushwa Ijumaa ya wiki hii ndani ya viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam na mastaa kibao wa muziki kutoka pande za Marekani na Jamaika.
Mashabiki wa Bongo watapata fursa ya kuwashuhudia lauvu na kujirusha na mastaa wa muziki kutoka Marekani kama Joe Thomas na kundi zima la Boyz II Men, huku Tanto Metro & Devonte na Tanya Stephens kutoka Jamaika wakiangusha ma-dancehall ya kutosha.
Waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Entertainment Masters (EM), wamesema katika taarifa yao kuwa maandalizi yote yako sawa ikiwemo wasanii hao kutamka kupitia luninga kuwa ni kweli wako njiani kudondoka ‘Tzee’. Kwa upande mwingine steji zitaanza kuvamiwa majira ya saa moja usiku, huku mashabiki wakizama ndani kwa viingilio vya shilingi lakini moja (VIP A), elfu hamsini (VIP B) na elfu ishirini sehemu ya kawaida.
“Hiyo ni kwa wale watakaokata tiketi zao mapema, watakaokatia getini siku ya tamasha watalipa shilingi lakini moja na elfu ishirini (VIP A), Elfu sitini (VIP B) na elfu thelathini, kawaida. Niimani yetu kwamba wewe mpenda burudani na shabiki utakuwa wakati wako wa kujiachia na mastaa hao”, walisema waandaaji.
*************************************
Naomi Campbell: Hii ni too much, midume zaidi ya 40!Ebwana Dah! Kutoka kunako mtandao wa ‘intaneti’ unaodili na uhusiano wa kimapenzi wa mastaa mbaliombali wa kiwanja tunaambiwa kwamba, mwanamitindo maarufu dunia, Naomi Campbell amewahi kujiachia na mastaa wa kiume zaidi ya 40, hii sasa ‘tu machi’.
Kwa mujibu wa mtandao huo, akiwa na umri wa miaka 38 hivi sasa Naomi amewahi kuwa na uhusiano na David Evans, Enrique Palacio, Francesco Carrozzini, Gabriel Byrne, Guy Laliberte, Johnny Depp, Kermit Nasser, Kevin Costner, Lewis Hamilton, Luca Orlandini, Marcus Elias na Muhammad Al Habtoor.
Wengine ni Pedro Diniz, Robert Goode, Sean Kanan, Sean Penn, Sergio Marone, Sylvester Stallone (Rambo), Joaquin Cortes, Mike Tyson mwaka 1987 - 88, Robert De Niro (1991 - 92), Eric Clapton (1993), Adam Clayton
(1993 - 94), Prince Albert II (1994 - 97), Chris Paciello (1995), Leonardo DiCaprio (1995) na Max Biaggi (1997).
Naomi hakuishia hapo, aliendelea kukandamiza raha na mastaa kama Joaquin Cortez (1997 - 98), Marcus Schenkenberg (1998), Flavio Briatore (1998 - 03), Joseph Fiennes (2000 - 01), Robbie Williams (2001),
Damon Dash (2001), Doug Band (2002), Puff Daddy (2002 - 03), Colin Farrell (2002), Matteo Marzotto (2003 - 05), Tommy Lee (2004), Usher Raymond (2004), Badr Jafar (2005 - 06) na Rolando Pintos (2007),
Pia Naomi alijiachia na Terrence Howard (2007), Gerard Butler (2007), Andre Balazs (2007), Hugo Chavez (2007),
Vladislav Doronin ambaye ndiyo yuko naye hivi sasa. Je, akitoka hapo atadondokea kwa dume gani? Ebwana Dah! Naomi anatisha.
4 comments:
Duh hiyo Ku** au bakuli sasa?!!!!
wewe unaanza kugeuza blogu yako ze utamu sasa...utatuboa sasa ivi
Huyo Naomi hana tofauti na changu eti.
Ngoma (ukimwi) haiogopi ustar... anaelewa hilo?
Post a Comment