Tuesday, January 22, 2008

ULIZA SWALI LINGINE !



Rais wa Tanzania katika mapumziko yake ya kila Christmas alipokwenda nyumbani kwake huko Masasi, Mkoani Mtwara kwa ndege ya Serkali alizuru mojawapo ya Day Secondary Schools za hapo mjini na kutoa fursa kwa Wanafunzi kumwuliza maswali yo yote.

RAIS: Nani atafungua dimba?


MASUMBUKO: Viongozi wa Serkali na wa Vyama vya Siasa wanatuambia kuwa Serkali ya Tanzania HAINA DINI. Lakini mbona ofisi zote za Serkali zinafungwa na Wafanyakazi wote Serkalini wanalazimika KUPUMZIKA KILA JUMAPILI?


RAIS: Uliza swali lingine.


MASUMBUKO: Swali la nyongeza; Hivi ni kweli nayo JUMAMOSI ilipitishwa Bungeni iwe pia siku ya mapumziko minajili ya KUWAWEZESHA NA WASABATO wapumzike?


RAIS: Mtoto mwingine?


CHAUSIKU: Katika Awamu ya Tatu kitabu maarufu kiitwacho "MWEMBECHAI Killings and the Political Future of Tanzania" kilipigwa marufuku kuuzwa na kuingizwa humu Nchini na hadi leo hakiruhusiwi kuonekana. Kisa? Tunanong'onezwa kuwa eti ni kwa sababu Kitabu hicho kinawakashifu mashabiki wazawa wa pale "MWEMBE-YANGA", Temeke - hiyo ni sahihi?


RAIS: Na swali la lala-salama nani atauliza?


CHAUSIKU: Hapa nchini Makanisa yote yana Makao Makuu (Headquarters) nje ya Tanzania na yanaletewa misaada ya hali na mali mda wo wote na miaka yote tokea Ukoloni .


Kulikoni misaada ya pesa inayoletwa kuboresha au kujenga Misikiti upya (ambayo maskini kuli hali mingi ni ya udongo na nyasi) INAZUIWA - kunradhi Mhadham Rais, eti ni kutokana na Madrassah zinazoendeshwa humo zinaeneza 'ugaidi'?


BREAKING NEWS!!

Inasemekana Masumbuko na Chausiku 'wametoweka' nyumbani kwao siku ile ile waliporejea kutoka shuleni na 'kuchukuliwa' na watu wanaodhaniwa ni 'Makachero' na mpaka sasa hawajulikani walipo!

JUMANNE KISHOKAH,
DAR ES SALAAM
TANZANIA

NOKIA MOBILE PHONE WITH CAMERA ONLY 4000/=

YOU ARE WHA YOU EAT!


LISHE SAHIHI INAVYOWEZA KUKUEPUSHA NA SARATANI

Wataalamu wa masuala ya afya wanaamini kuwa robo ya vifo vyote vinavyotokana na saratani husababishwa na ulaji vyakula usiosahihi na unene wa kupita kiasi (obesity).

Aidha, inaaminika kuwa milo yetu ya kila siku inachangia kwa kiasi kikubwa saratani za aina mbalimbali zikiwemo za tumbo, mdomo na matiti.

Hata hivyo, unaweza kupunguza hatari ya kupatwa na saratani kwa kuzingatia ulaji sashihi kama ambavyo tumekuwa tukieleza kila wiki katika makala yetu na kama itakavyosisitizwa tena leo katika makala haya.

Wataalamu wetu wanashauri watu wapende kula vyakula vyenye ‘faiba’ nyingi (ufumwele), kama matunda, mboga za majani na kula kwa uchache sana nyama nyekundu na vyakula vya kusindikwa. Vyakula vya kwenye makopo vinapigwa vita kutokana na kemikali zinazotumika kuhifadhia vyakula hivyo.

Katika makala ya leo tutajaribu kueleza ni kwa kiasi gani vyakula unavyokula vinaweza kukuongozea hatari ya kupata saratani. Aidha tutaelezea ni ulaji upi sahihi unaoweza kukuepusha na saratani.

UHUSIANO KATI YA LISHE NA SARATANI.
Uhusiano kati ya saratani na lishe ni suala tete na gumu kulibainisha. Hali hii inatokana na ukweli kwamba milo yetu ina mchanganyiko wa vyakula vingi na virutubisho mchanganyiko. Vyakula vingi huchangia hatari ya mtu kupata saratani, hasa vinapochanganywa na vingine, ingawa wakati mwingine mtu huweza kupata saratani kwa kurithi vinasaba ‘genes’.

Wanasayansi wengi wanafanya kazi usiku na mchana ili kujua ni vyakula gani hasa vinaweza kutulinda dhidi ya saratani na vyakula vipi vinaweza kutusababishia satarani, baadhi ya tafiti zimeshaweza kulijua hilo na tafiti zaidi bado zinaendelea kufanywa.

Kwa sasa, vipo vyakula vinavyofahamika kwa ubora ambavyo kila mtu anapaswa kuvila. Tunaelewa pia kuwa mlo sahihi unasaidia kudhibiti uzito wa mwili ambao ukidhibitiwa vizuri, unamuondolea mtu hatari ya kupata saratani za aina mbalimbali.

MATUNDA NA MBOGA MBOGA
Ulaji wa matunda na mboga kwa wingi kunapunguza hatari ya mtu kupata ugonjwa wa saratani, hasa saratani ya viungo vya kwenye mfumo wa kupitishia chakula, kama vile mdomo, tumbo na njia ya haja kubwa. Hata hivyo matunda na mboga vinaweza visiondoe kabisa hatari ya mtu kupata saratani zinazosababishwa na ‘homoni’ kama saratani ya ziwa na kizazi.
USHAURI SAHIHI: Penda kula angalau milo mitano ya matunda kwa siku na mboga tofauti tofauti. Ulaji wa matunda ya rangi tofauti husaidia kupata aina mbalimbali za vitamini na madini ambayo yataupa kinga mwili wako dhidi ya maradhi mbalimbali.

NYAMA
Ulaji kidogo wa nyama nyekundu na za kusindika husaidia kupunguza hatari ya kupata saratani ya utumbo, kwani vyakula hivyo si vya kupenda kula kwa wingi, japo ni vitamu mdomoni.

Kuwa na tabia ya kupenda sana kula nyama nyekundu na za kusindika kunaongeza hatari ya mtu kupata saratani ya tumbo. Nyama nyekundu zinajumuisha pia nyama ya nguruwe, iwe ya vipande au kusagwa pamoja na ‘soseji’. Nyama nyeupe, kama vile ya kuku na samaki hazina hatari.

USHAURI: Kula kiasi kidogo sana cha nyama nyekundu na za kusindika. Badilisha kwa kula maharage au kunde badala ya nyama. Unapopika nyama, tumia joto kiasi au mvuke, upikaji nyama kwa moto mkali mpaka inaungua kunaweza kuzalisha kemikali za saratani.

SAMAKI
Ulaji kwa wingi wa samaki kunaweza kukupunguzia hatari ya kupata saratani. Pendelea kula samaki zaidi kuliko nyama nyekundu au za kusindika kama tulivyozianisha hapo juu. Samaki wa kuoka, kuchemsha ni bora zaidi.

VYAKULA VYENYE CHUMVI
Vyakula vyenye chumvi nyingi au vyakula vilivyohifadhiwa kwa chumvi, vinaongeza hatari ya mtu kupata satarani ya utumbo na koo. Hata hivyo, tafiti zingine zinaonesha kuwa chumvi ya mezani inayotumika kupikia au kuongezea ladha haina uwezekano wa kuchangia saratani, lakini chumvi nyingi huongeza shinikizo la damu na hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na hatimaye kiharusi.

USHAURI: Usipende kula vyakula vyenye chumvi nyingi au vile vilivyohifadhiwa kwa kutumia chumvi. Unaponunua vyakula vya kusindika, kagua kiasi cha chumvi kulichomo. Chumvi inaweza kufichwa mahali ambako hukutegemea, hasa kwa vyakula vinavyochanganywa na sukari.

VYAKULA BORA
Vyakula bora vyenye kiwango kikubwa cha ‘faiba’ (ufumwele) hupunguza hatari ya mtu kupatwa na satarani. Vyakula hivyo ni pamoja na matunda, mboga mboga, nafaka zisizokobolewa na mikate inayotengenezwa kutokana na ngano isiyokobolewa (whole bread), mchele mweusi, kunde, n.k.

MAFUTA
Mafuta ni muhimu kwa mwili wa binadamu, lakini haishauriwi mtu kupenda kula vyakula vyenye mafuta mengi, hasa mafuta ya wanyama ambayo siyo mazuri kiafya. Kwa ujumla kanuni ya ulaji sahihi ni kula matunda na mboga kwa wingi, vyakula vitokanavyo na nafaka zisizokobolewa na jamii yote ya kunde na maharage, vyakula hivyo vimethibitisha kupunguza kwa kiwango kikubwa hatari ya mtu kupata saratani.

Monday, January 21, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Makamua: Nimewahi kutongozwa na jimama, tena mwenye nyadhifa zake.

Kwa mara ya kwanza tangu ilipoanzishwa, 'Hot Corner' ilikutana uso kwa uso na staa wa Bongo, Mack Paul Sekimanga a.k.a Makamua, tofauti na siku nyingine ambapo hupiga stori na watu maarufu kwa njia ya simu.

'Dogo' akiwa ni mwanafunzi katika Sekondari ya Makongo, Dar es Salaam ambaye pia anafanya kazi ya kuelimisha na kuburudisha jamii kupitia sanaa ya muziki wa kizazi kipya, alikutana na maswali 'hot' kutoka kwa mwandishi Catherine Kassally.


1. Kwa nini unajiita Makamua?

Kwasababu nilijigundua ninauwezo mkubwa wa kukamua, namaanisha kuimba, kitu kilichowafanya washikaji zangu pia waniite hivyo.

2. Nani aliyefanya kazi kubwa ya kukuinua mpaka leo uko juu katika game?

Yaani nawashukuru sana wazazi wangu japo siku za mwanzo walikuwa wananibania, lakini baada ya kuona matunda yangu kila mmoja ananipa sapoti ya kutosha hasa mama yangu mzazi nampenda sana.

3. Inasemekana unauhusiano wa kimapenzi na msanii Enika. Je, hilo linaukweli?

Makamua: Inawezekana mimi kutembea na Enika, kwani ni mtoto wa kike mwenye mvuto hasa kwangu, sijui nieleze vipi. Ila napenda mjue namzimia kuliko maelezo.

4. Ulishawahi kutongozwa na jimama (shugamami) yoyote?
Ndiyo, niliwahi kutongozwa na shugamami tena mwenye wadhifa mkubwa serikalini, lakini nilimchomolea kwasababu napenda kuwa na rafiki au mchumba wa rika langu.

5. Kama ukijaaliwa kuwa na familia yako ungependa kuwa na watoto wangapi na uzae na mwanamke wa aina gani?

Ningependa kuwa na watoto wawili, si unajua maisha yanabana sana, pia ningependa kuzaa na mwanamke ambaye ananiheshimu, anajiheshimu yote hayo yanawezekana kwa mwanamke ninayempenda.


Madee Kuomba msamaha

Baada ya kunusurika kupigwa na mashabiki katika baadhi ya shoo alizofanya hivi karibuni, pale alipoimba wimbo wake 'Hip Hop haiuzi' msanii Hamad Ally 'Madee' kutoka ndani ya Familia ya Tip Top Conection, yenye maskani yake Manzese, Dar es Salaam yupo katika ziara ndefu akiwaomba mashabiki hao wamuelewe, Violet Mushi alipiga naye stori.

Akipiga stori na Abby Cool & MC George Over The Weekend, kwa njia ya simu msanii huyo ambaye hivi sasa yuko Kanda ya ziwa akiendelea na ziara hiyo alisema kwamba anachojaribu kufanya ni kuwaomba mashabiki waelewe vitu alivyoimba kunako traki hiyo.

"Watu wamekuwa wakiupokea wimbo huo katika fikra potofu, kitu ambacho kinaniweka katika wakati mgumu, ndiyo maana nataka kuwaelimisha kwamba mimi kama msanii nimefikisha ujumbe ili ufanyiwe kazi, nilichofanya ni kukusanya mawazo ya mashabiki mbalimbali na kuyatungia wimbo, siyo kama nilikurupuka nikarekodi wimbo huo, mbona mimi pia nafanya Hip Hop?', alihoji Madee.

Mpaka sasa msanii huyo ambaye pia baadhi ya kazi zake zinapatikana ndani ya albamu ya Tip Top Compiration yenye mchanganyiko wa kazi za wasanii wa familia hiyo, ameshazunguka sehemu kibao Tanzania Bara ikiwemo Singida, Nzega, Kahama, Musoma, Kigoma, Mwanza na kwingine akiwa na wakali wengine kama PNC na Kassim kwa ajili ya shughuli hiyo.
Tollywood kuisapoti muvi ya Imbwiga

Kampuni ya Tollywood ya Dar es Salaam ambayo inakuja juu katika tasnia ya usambazaji wa muvi Bongo, imejitolea kuisimamia filamu kali na ya kutisha, Imbwiga inayotarajiwa kudondoka mtaani hivi karibuni.

Stelingi wa muvi hiyo, Majani Kasoga Nsyuka, aliyepata kutamba ndani ya filamu ya Nsyuka, ameiambia safu hii kwamba, ubora wa kazi hiyo ndiyo umemfanya apate shavu Tollywood na kwamba ana uhakika ataliteka soko la Bongo.

"Kwa wale mashabiki waliopata kuniona kwenye filamu ya Nsyuka, watakubaliana na mimi kwamba nimekuja tofauti sana. Ndani ya muvi hiyo nimecheza sehemu tatu tofauti, yaani Imbwiga ambao ni mzimu wa watu wa Musoma, Bob Kijiti ambaye ni kijana wa mtaani na Majani mzimu wa Kijiti," alisema.

Aidha ndani ya muvi hiyo mashabiki watapata fulsa ya kushuhudia vitu vipya kabisa katika sanaa ya filamu Bongo ikiwemo ile sehemu ambayo Bob Kijiti amecheza kama Majani, yaani mtu mmoja ambaye anaonekana kama watu wawili tofauti. Kwa kifupi ni bonge la picha ambalo wewe msomaji na shabiki wa filamu za Kibongo hutakiwi kulikosa.

Friday, January 18, 2008

NANI ALISEMA NI TUZO YA OSCAR?




Baadhi ya Wasomaji wamezua mjadala usiokuwepo kuhusu tuzo ya Kanumba, hebu tuisome habari hii iliyoandikwa kuelezea tuzo hiyo, sioni mahali palipoandikwa kuwa KANUMBA AMEPEWA TUZO YA OSCAR...labda ni macho yangu..!

Msanii wa filamu nchini, Steven Kanumba mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akimwaga chozi la furaha nchini Marekani baada ya kupewa tuzo ya Best Tanzania Hollywood Achievement, kutoka Kampuni ya Universal Hollywood ya nchini humo.

Kanumba ambayealiwasiliana na mwandishi wetu kwa njia ya barua pepe alisema kuwa, amefurahi sana na hakuamini macho yake alipotembea juu ya red carpet (kapeti jekundu) kupokea tuzo hiyo.

“Kaka nina furaha sana usiku huu wa leo, nimepewa tuzo nyingine kama Best Tanzania Achievement Actor yaani muigizaji mwenye mafanikio kutoka Tanzania iliyotolewa na Kampuni ya Universal Hollywood, nimetembea juu ya kapeti jekundu huku machozi yakinitoka, kusema kweli siamini kilichotokea,” alisema Kanumba.

Alisema mara baada ya kumaliza zoezi la kupokea tuzo, waliandaliwa sherehe ya nguvu kwenye Ukumbi wa Aqua Lounge, Los Angeles ambapo ilihudhuriwa na mastaa kibao wa Hollywood.

Msanii huyo alisema kuwa, kwa muda mfupi aliokaa huko amejifunza mengi na ameweza kujichanganya na baadhi ya mastaa wanaoigiza sinema za kutisha duniani kama anavyoonekani akiwa amepozi nao kwenye picha ya ukurasa wa mbele.

Hii ni tuzo ya pili kwa msanii huyo kutunikiwa kutoka Marekani ambapo ya kwanza ni ya Johnwyne International Award.

Kanumba yuko nchini Marekani kwa takriban miezi mitatu sasa kwa mwaliko wa Kampuni ya Johnwyne ya Hollywood. (Source: www.globalpublisherstz.com)