Thursday, January 29, 2009

A.Y huyoo kiwanja

Jumatano ya wiki hii, ShowBiz ilikuwepo pande za uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam na kumshuhudia msanii Ambwene Yesaya ‘AY’ akiwa kwenye mishe mishe za safari ya Uingereza (kama anavyoonekana pichani) ambako anakwenda kupiga shoo kadhaa kabla ya kureja Bongo na kuendelea na harakati nyingine.

Mbali na AY, msanii Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ anatarajia kuondoka leo kuelekea nchini humo ambako ataungana na swahiba wake huyo katika shoo, lakini yeye atabaki kwa ajili ya kuendelea na masomo.


No comments: