Bushoke: Kupoteza Kanda ya Ziwa na mastaa kibao
Baada ya kudondosha albamu yake, ‘Dunia Njia’ kitaani, msanii Ruta Maximilian Bushoke tayari ameanza mishemishe za uzinduzi ili kuwaeleza mashabiki wake nini kilichomo ndani ya albamu hiyo.
Akipiga stori na ShowBiz msanii huyo alisema kwamba, kwa kuanza yeye pamoja na timu ya wasanii kibao watavamia Kanda ya Ziwa ambapo Jumamosi ya Februari 7, mwaka huu wataangusha bonge la shoo ndani ya ukumbi wa Yatch Club, jijini Mwanza.
“Siku itakayofuata, yaani Februari 8 tutaitambulisha albamu hiyo ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba. Katika ziara hiyo nitakuwa na timu ya wasanii kibao wakiwemo Chid Benz, Blue, Ngwea, Squeezer, Maunda Zorro, Steve na wengine kibao bila kuvisahau ‘vichwa’ vinavyounda bendi yangu,” alisema Bushoke.
Albamu hiyo ya Bushoke ina ngoma zaidi ya kumi na imedondoka kitaani ikiwa kunako CD na kanda za kawaida.
******
Fella: Hii ndiyo ngoma yake
Baada ya kuenea kwa uvumi kwamba, meneja wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Fella ameamua kuingia studio na kurekodi wimbo wake binafsi, kisha kiongozi huyo kuibuka na kuweka wazi kuhusu hilo, ShowBiz ilikwenda hewani kumtafuta ili kuwafahamisha wasomaji na mashabiki wa kundi lake kwa ujumla nini hasa alichokiimba katika ngoma hiyo.
Bila kusita Fella alitoa ushirikiano wa kutosha kwa kusema kwamba ameamua kuingia studio ili kuwaeleza mashabiki na wapenzi wa kundi hilo ukweli halisi tofauti na baadhi ya watu wanavyodhani, hasa wanapopata taarifa ambazo siyo za kweli kutoka kwa baadhi ya wasanii waliyowahi kupitia TMK Family.
Ishu nyingine kubwa ni kwamba, safu hii ilifanikiwa kuisikiliza ngoma hiyo na kwa mara ya kwanza kabisa kabla hata haijaanza kwenda hewani kupitia vituo vya redio, wewe msomaji utaisoma kupitia hapa (kulia) ndiyo maana tukaanza na maneno ‘Exclusive’.

Ishu nyingine kubwa ni kwamba, safu hii ilifanikiwa kuisikiliza ngoma hiyo na kwa mara ya kwanza kabisa kabla hata haijaanza kwenda hewani kupitia vituo vya redio.
Jay: Auanza 2009 vibaya, Benz lake lapata ajali
Mwaka huu wa 2009 umeanza vibaya kwa mkali wa Hip Hop, Joseph Haule ‘Prof. Jay’ kwani mwishoni mwa wiki iliyopita gari lake aina ya Benz lilipata ajali na kuharibika vibaya.
Gari hilo lilipata tafrani hiyo maeneo ya Muhimbili, Dar es Salaam baada ya tairi za mbele zote kupasuka na hatimaye kuchomoka wakati Dj wa Jay, Choka alipokuwa anatoka pande za fire kununua luku huku akiwa kwenye kasi ndefu.
ShowBiz imezipokea taarifa hizo kwa masikitiko, inatoa pole kwa Prof. Jay japo hakuwemo ndani ya gari hilo, bila kumsahau Dj Choka ambaye alikuwa akiendesha gari hilo na kufanikiwa kutoka salama baada ya kuivaa nguzo iliyokuwa kwenye geti la nyumba moja maeneo hayo.

********
Fella: Ngoma iko tayariBaada ya kuenea kwa uvumi kwamba, meneja wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Fella ameamua kuingia studio na kurekodi wimbo wake binafsi, kisha kiongozi huyo kuibuka na kuweka wazi kuhusu hilo, ShowBiz ilikwenda hewani kumtafuta ili kuwafahamisha wasomaji na mashabiki wa kundi lake kwa ujumla nini hasa alichokiimba katika ngoma hiyo.
Bila kusita Fella alitoa ushirikiano wa kutosha kwa kusema kwamba ameamua kuingia studio ili kuwaeleza mashabiki na wapenzi wa kundi hilo ukweli halisi tofauti na baadhi ya watu wanavyodhani, hasa wanapopata taarifa ambazo siyo za kweli kutoka kwa baadhi ya wasanii waliyowahi kupitia TMK Family.
Ishu nyingine kubwa ni kwamba, safu hii ilifanikiwa kuisikiliza ngoma hiyo na kwa mara ya kwanza kabisa kabla hata haijaanza kwenda hewani kupitia vituo vya redio.
Jay: Auanza 2009 vibaya, Benz lake lapata ajali
Mwaka huu wa 2009 umeanza vibaya kwa mkali wa Hip Hop, Joseph Haule ‘Prof. Jay’ kwani mwishoni mwa wiki iliyopita gari lake aina ya Benz lilipata ajali na kuharibika vibaya.
Gari hilo lilipata tafrani hiyo maeneo ya Muhimbili, Dar es Salaam baada ya tairi za mbele zote kupasuka na hatimaye kuchomoka wakati Dj wa Jay, Choka alipokuwa anatoka pande za fire kununua luku huku akiwa kwenye kasi ndefu.
ShowBiz imezipokea taarifa hizo kwa masikitiko, inatoa pole kwa Prof. Jay japo hakuwemo ndani ya gari hilo, bila kumsahau Dj Choka ambaye alikuwa akiendesha gari hilo na kufanikiwa kutoka salama baada ya kuivaa nguzo iliyokuwa kwenye geti la nyumba moja maeneo hayo.
******
No comments:
Post a Comment