
Siku chache baada ya kudondoka kutoka pande za UK (Uingereza) alipokuwa akipiga shoo na swahiba wake, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA', msanii Ambwene Yesaya 'A.Y' ameiambia ShowBiz kwamba kazi iliyopwapeleka kule wameimaliza salama.
Ambwene alisema kwamba walikuwa na shoo mbili, ya kwanza ilifanyika katika Jiji la London, huku ya pili ikiangushwa Leads na baada hapo yeye alirudi Bongo na kumuacha FA akiendelea na shule. "Shoo zote tulifanya katika kumbi za burudani, tunashukuru mashabiki wengi hasa Wabongo walitoa sapoti ya kutosha".
Aidha, msanii huyo alisema kwamba ndani ya shoo hiyo kijana Mwana FA aliwarusha mashabiki kwa kuonesha uzalendo wa kutosha, pale alipopanda stejini na fulana yenye picha kubwa ya Rais Kikwete, kisha akawaambia watu kwamba, JK anaanza, Obama anafuatia kitu ambacho kiliwavutia mashabiki wengi ambao mwisho wa burudani walionekana wakipiga naye picha.
"Lakini mbali na yote kila kitu huwa kina matatizo yake, kwa kifupi promota wetu alitaka kutufanyia siyo, kwanza tulipofika alitaka tukalale nyumbani kwake kitu amabcho nilikipinga kwasababu sisi tulikuwa kibishara zaidi, siyo familia yake. Baadaye alipoona msimamo wetu haubadiliki akatutafutia hoteli. Baada ya shoo hiyo natarajia kwenda kupiga ishu nyingine mbili Marekani, Machi 5, mwaka huu katika miji ya Washington na Miniapolis itakayokuwa Machi 7," alisema A.Y.
*****************************************************************
Baada ya kusota kwa muda akitafuta njia ya kutoka kupitia game ya muziki, aliyekuwa mshiriki wa shindano la Project Fame 2008, Hemed Suleiman amejikomboa baada ya kuachia ngoma yake ya kwanza yenye jina la 'ninachotaka' na kuonesha kufanya vyema kunako chati mbalimbali za muziki zikiwemo Bamiza, Imelda Mtema alicheki nae.
Akipiga stori na ShowBiz, Hemed alitamka kwamba ngoma hiyo imefanyika kupitia studio za Sei Record na kwamba siku chache zijazo ataachia kazi nyingine ambayo tayari imekwishakamilika.
"Kazi hizo zitaitambulisha albamu yangu ya kwanza tangu nilipotambulika kupitia shindano la Project Fame ambayo itakwenda kwa jina la 'Brown Colour' ikiwa na ngoma zaidi ya 11. Ndani ya albamu hiyo nimewashirikisha wasanii wachache, pia nimerekodi katika studio tofauti ili kupata l1adha zaidi ya moja," alisema Hemed.
****************************************************************
3 comments:
Huyo dada anae onekana kwenye picha hiyo hapo juu na wasanii wetu AY na Mwana FA anaitwa SPORAH na anatalk show yake iitwayo SPORAH SHOW nchini Uingereza na unaweza angalia kipindi chake kila Jumatatu saa nne na nusu usiku kupitia BEN TV Channel 184 UK time. Anajitahidi sana na Mungu ambariki.
Yes Huyo Dada Anaitwa Sporah na ana Tv show yake inaitwa ZE SPORAH SHOW!! Kweli anajitahidi sana lakini mwambienio ajaribu kujichangaza na watu. TV Show yake ni nzuri sana kwakweli.
Ila Mbona anajificha sana?? Au ndo AY na AF wananyemelea?
Wote niwasanii lakini. Kila la kheri dada.
Yes Anajitahidi, ila aache kunata bwana.
Post a Comment