Monday, February 2, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

maunda zorro
Bushoke
Chidi Benz, Maunda kwenye msafara wa Bushoke

Pamoja na kutangaza kuachia ngazi kwenye game ya muziki wa kizazi kipya, msanii Rashidi Mwakwilo ‘Chid Benz’ (pichani juu) ni miongoni mwa wakali wa sanaa hiyo watakaokuwa kwenye msafara wa kijana Rutta Maximilian ‘Bushoke’ utakaoelekea Kanda ya Ziwa kwa ajili ya utambulisho wa albamu yenye jina la ‘Dunia njia’.

Akipiga stori na Abby Cool & MC George Over The Weekend, Bushoke alisema kwamaba, anajisikia fahari kuwa na Chid Benz katika ziara ya uzinduzi wa albamu yake hiyo utakaoanzia ndani ya Ukumbi wa Yatch Club, Mwanza Februari 7, mwaka huu kwasababu jamaa bado yuko juu na mashabiki wake hawajaamini kama kweli anaachia ngazi.

Aidha, Bushoke ambaye hivi sasa anafanya kazi zake akiwa na bendi alisema kuwa, baada ya Yatch Club, siku itakayofuata yaani Februari 2 shoo itahamia ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba. “Mbali na Chid Benz msafara huo utakuwa na mastaa wengine kama Ngwea, Blue, Squeezer, Steve na Maunda Zorro, pia baadhi ya wasanii wa Kanda ya Ziwa watapewa nafasi ya kupiga shoo siku hiyo”.

Albamu ya mchizi ‘Dunia njia’ ambayo ilidondoka kitaani mapema Januari mwaka huu, ikiwa kwenye CD na ‘tape’ za kawaida ina ngoma zaidi ya kumi zikiwemo Wanashindwa lala, Chupa ya Coca, ‘Usiende mbali’ aliyoshirikishwa na Juliana Kanyomozi wa Uganda na nyingine kibao, kwa kifupi ni albamu ambayo imeshiba.
Miguu Bomba
Baada ya kumalizika kwa shindano la kumtafuta staa wa kike mwenye mdomo wenye mvuto wa kimapenzi ‘Nani anadatisha?’, kisha Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kuibuka na ushindi, Abyy Cool & MC George Over The Weekend inakuletea mpambano mwingine wa nguvu utakaokwenda kwa jina la ‘Miguu Bomba’.

Shindano hili litawakutanisha mastaa wa kike kibao na kati yao atatafutwa mwenye miguu yenye mvuto kisha wewe msomaji utatuambia ni miguu ya nani ina mvuto zaidi. Kabla hatujaanza zoezi hilo wiki ijayo, tunatoa nafasi kwako wewe msomaji na mpenzi wa safu hii ututajie jina la staa wa kike ambaye unadhani anastahili kuingia katika mpambano huu.

Nyoshi: Wazee wa Ngwasuma tutavamia Segerea wiki hii

Baada ya kufunika kunako shoo ya Promosheni ya Jishindie Pajero iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Msasani Club jana, Bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma,’ Jumatano ya keshokutwaa wataangusha shoo nyingine ndani ya Ukumbi wa Rufita Executive uliyopo pande za Segerea, Dar es Salaam.

Akipiga stori na safu hii, kiongozi wa bendi hiyo, Nyoshi El Sadat (pichani juu) alisema kwamba mwaka huu wa 2009 wamepania kufanya mambo makubwa zaidi ikiwemo kufanya shoo nyingi na kudondoka na vitu vipya katika tasnia ya muziki wa dansi.

“Hivi sasa tuna muda mchache sana wa kupumzika, lakini tunafurahi kwasababu mashabiki wetu wanatuhitaji kwa wingi na sisi kwasababu tupo kwa ajili ya kufanya kazi tutaendelea kuangusha shoo tu ili Ngwasuma iendelee kuwa juu. Watu watapata fursa ya kushuhudia laivu shoo ndani ya Rufita kwa kiingilio cha shilingi 4,000 tu,” alisema Nyoshi.
Bwana Misosi: Mapenzi ya Kibongo wizi mtupu!

Joseph Rushahu ndiyo jina lake, Bw. Misosi linamtambulisha akiwa kazini kunako game ya muziki wa kizazi kipya. Pande za Sinza Makaburini, Dar es Salaam ndiyo anafanya maisha yake kwa sasa baada ya kutoka nyumbani kwao Tanga, Edina Katabalo na Shufaa Lyimo walipiga naye stori.

Mchizi ambaye sasa anasomeka kupitia ngoma yake, ‘Nimesomeka’ alisema na safu hii kwamba, mapenzi ya Wabongo wengi ni wizi mtupu tofauti na ilivyo kwa wenzetu katika nchi za mbali. “Imenilazimu kusema hivyo kwasababu nimeshashuhudia na kusikia wanaume au wanawake wengi wanavyofanyiwa vituko na wapenzi wao, kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza wengi,” alisema. Aidha, Misosi alisema kuwa wapendandao wengi, hasa wasichana wa dunia ya leo hawana mapenzi ya kweli kwa wapenzi wao zaidi ya kuchungulia mkwanja na maslahi mengine ya juu.

“Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyonifanya nisijiingize katika ishu za mapenzi zaidi ya kufikiria sanaa yangu ya muziki. Hivi sasa nimerudi kivingine kabisa, kuanzia muonekano mpaka mashairi, watu walizoea kuniona nina rasta kichwani lakini leo hii nimenyoa nywele, nimechoka kutafsiriwa vibaya na baadhi ya binadamu ambao walidhani navuta bangi,” alisema.
compiled by mc george

No comments: