Wednesday, March 18, 2009

JE, UMEWAHI KUFANYA ENEMA?

HAPO zamani, niliwahi kuandika makala kuhusu somo tajwa hapo juu, somo ambalo liligusa wasomaji wengi wa gazeti hili. Katika simu kadhaa ambazo nimekuwa nikipokea kutoka kwa wasomaji wakiomba msaada wa masuala mbalimbali, hujikuta nikilazimika kuwaeleza pia kuhusu suala la Enema, lakini wengi wao wameonekana kutoifahamu.

Hivyo leo nimeamua kuanza kuandika tena mfululizo wa makala haya kuhusu suala hili, ambalo ndilo msingi wa afya bora na uhai wa kila mmoja wetu. Inawezekana hata wewe ukawa unasikia kwa mara yako ya kwanza neno ENEMA, lakini napenda kukuhakikishia kwamba neno hili lipo tangu enzi za mababu zetu na ni maarufu sana miongoni mwa kizazi cha babu au bibi zetu waliyopo hai hivi sasa.

Babu zetu walidumisha sana enema katika maisha yao ya kila siku katika familia nzima, kwa kufanya enema mara kwa mara waliweza kujiepusha na maradhi mengi na kuishi na afya njema, wengine wakiwa wangali hai hadi sasa wakiwa na nguvu zao katika umri wa miaka 80 au 90.
Kwa lugha nyepesi kabisa, Enema ni njia ya asili (natural way) ya kusafisha na kuondoa sumu (cleansing and detoxifying) kwenye utumbo mpana kwa kutumia maji ambayo mtu huyapitisha kupitia sehemu zake za nyuma. Mtu anaweza kujisafisha mwenyewe kwa kutumia vifaa malaumu (Enema Kit) au kwa kwenda kwenye kliniki maalumu, ambazo kwa hapa nchini sijawahi kusikia kama zipo, lakini katika nchi zilizoendelea kliniki za aina hii zipo nyingi.

Njia hii ina wafaa sana wale ambao hawewezi kunywa maji mengi asubuhi kwa utaratibu tuliokwisha ueleza, kwa lengo la kusafisha mifumo yao ya mwili, ukiwemo utumbo mkubwa ambao ndio unaotakiwa kuwa safi wakati wote. Kunywa maji kama tiba, ni njia moja ya kusafisha utumbo wako mkubwa, lakini kama huwezi njia hiyo ya kunywa, basi huna budi kufuata njia hii, lengo likiwa ni kuhakikisha utumbo wako mkubwa unakuwa safi.

KUNA ULAZIMA GANI WA KUFANYA ENEMA?
Katika tasinia hii ya Enema, kuna msemo mmoja maarufu sana usemao Death Begins at the Colon (kifo huanzia kwenye utumbo mkubwa). Msemo huu una maana kwamba chanzo cha maradhi mengi yanayosababisha vifo vya binadamu huanzia kwenye utumbo mkubwa pale unapokuwa mchafu na mazalia ya maradhi.

Inaelezwa na wataalamu wa afya kwamba utumbo mkubwa (large Intestine), unapokuwa mchafu, kila kitu hushindwa kufanya kazi yake ipasavyo, hata kama utakula lishe au virutubisho bora kiasi gani, haviwezi kukusaidia sana kiafya na hata utakapotumia dawa kujitibu na magonjwa, dawa haziwezi kufanya kazi yake sawa sawa, kwani njia zote huwa zimezibwa.

Itaendelea wiki ijayao…


1 comment:

Anonymous said...

DUUU ASANTE SANA MIMI NI MVIVU SANA KUNYWA MAJI TENA MAJI YA DENMARK SIO MATAMU KAMA YA KWETU YANA KALK BASI NDO KABISA KWA MTAJI HUU NITAKUNYWA MAJI SANA SANA DUUUU ASANTE ABDALLAH MRISHO