Monday, March 2, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ

Vivica Fox
Ne-Yo: DAH! KAJIACHIA MPAKA NA DEMU WA 50 CENT
Baada ya kuipokea ngoma yake yenye jina la ‘Miss Independent’ kwa mikono miwili na ambayo bado inafanya vyema hadi hivi sasa tangu ilipotoka mwishoni mwa mwaka jana, mashabiki wengi walitutumia ujumbe mfupi (SMS) wakitaka kufahamu mwanamuziki Ne-Yo Smith kutoka pande za Marekani amewahi kujiachia na mastaa wa kike wangapi?

Meseji za wasomaji ambao ndiyo wadau wakuu wa kurasa hizi zilitufanya tuzame ndani ya mtandao wa ‘Intaneti’ fasta na tulichobaini kuhusu Ne-Yo ilibidi tustaajabu, siyo kwamba mchizi amewahi kujiachia na mademu kibao bali ni jinsi alivyoweza ‘kujiramba’ na aliyewahi kuwa demu wa 50 Cent, mwanamitindo Vivica Fox, tabia ambayo wanayo mastaa wengi hata wa Kibongo.

Lakini pamoja na hilo, kwa mujibu wa mtandao wa ‘intaneti’ unaodili na uhusiano wa mastaa wa Ulaya, Ne-Yo amewahi kujirusha na mastaa wa kike wawili tu, yaani Vivica Fox na Jesse White. Akiwa na umri wa miaka 29 hivi sasa, mkali huyo wa ngoma ya Miss ‘Independent’ ambaye hivi sasa kaangusha remix yake akiwa na wasanii ‘Jamie Fox’ na ‘Fabulous’ alizaliwa October 18, 1979, huko Camden, AR na kupewa jina la Shaffer Chimere Smith.
**************************************
FEROUZ sasa ashusha pumzi na Mr. Polisi Man
Kutoka ndani ya studio za Bongo Records anakopigia kazi zake, msanii Ferouz Mrisho ‘Ferouz’ sasa anaonekana kupumua baada ya ngoma yakempya ‘Mr. Polisi man’ kuonesha dalili ya kumrudisha juu kama ilivyokuwa kwenye ‘Starehe’.

Mchizi ambaye hivi karibuni alikatiza pande za safu hii na kugonga picha mbili tatu mpya kama unavyomcheki huku akiwa na tabasamu la kutosha, siku kadhaa alikuwa kwenye wakati mgumu pale alipojaribu kuachia kazi mpya kadhaa bila mafanikio.

Mbali na hilo aliendelea kuandamwa na ‘midomo’ ya Wabongo wengi waliodai kwamba hata mkwanja uliokuwa unamilikiwa na msanii huyo umeingia mitini na kumuacha vibaya, kitu ambacho mchizi hakikumkatisha tamaa zaidi ya kuendelea kupambana na hatimaye kuibuka na ‘Mr. Polisi Man’ huku akiwaonesha mashabiki wake kuwa, voko bado zipo.

Huo ndiyo ukurasa mpya wa msanii huyo ambaye ameahidi makubwa zaidi siku kadhaa zijazo.

*********************************************
MBISHI REAL nje ya Nitoke vipi Squard
Baada ya kuonesha uwezo wa kutosha ndani ya ngoma, ‘Nimesomeka’ ya kwake Bwana Misosi, akiwa chini ya familia waliyoipa jina la ‘Nitoke Vipi Squard’, msanii Fredy Kaguo ‘Mbishi Reel’ anatarajia kutoka pembeni ya Squard hiyo na jiwe binafsi lenye jina la ‘Surprise’, Edna Katabalo aliangusha naye stori.

Akipiga stori na safu hii, Mbishi alisema kwamba, ngoma hiyo ambayo inazungumzia moja kati ya stori zake za kimapenzi (True Story) ipo kunako hatua ya mwisho kukamilika na siku chache zijazo itapanda hewani kupitia vituo kadhaa vya redio, ikifuatiwa na video yake.

“Kila kitu kuhusu kazi hizo kitakamilika leo (Jumatatu), mashabiki wangu wategemee mambo mazuri.Baada ya mishemishe hizo nitahamishia nguvu kwenye maandalizi ya wimbo wa kundi letu, ‘Nitoke Vipi Squad’ lenye jumla ya vichwa vitatu, mimi, Bwana Misosi na J Force,” alisema Mbishi.
#####################################
compiled by mc george

1 comment:

Anonymous said...

Huyu neyo mbona nasikia ni gay?????