Monday, March 9, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Bushoke, Ngwea watimkia chuoni Bagamoyo
Baada ya ziara ndefu kwa ajili ya kuinadi albamu yake mpya, ‘Dunia njia’, msanii Rutta Maximilian Bushoke na mchizi aliyekuwa naye bega kwa bega kwenye uzinduzi huo, Albert Mangwea ‘Ngwea’ wameamua kujitupa pande za Chuo cha Sanaa, Bagamoyo kwa ajili ya kuongeza maujanja zaidi katika game yao ya muziki, Edna Katabalo alipiga naye stori.

Akipiga stori na safu hii, Bushoke alisema kuwa yeye na Ngwea wameamua kurudi darasani kunako chuo hicho ili waweze kuongeza ufahamu zaidi katika sanaa ya muziki ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na ushindani uliopo kwenye tasnia hiyo hivi sasa, kwani wanaamini kwamba, bila elimu huwezi kufika kimataifa zaidi.

“Tumegundua kwamba bila elimu hatuwezi kufanya mambo kwa ufanisi zaidi, ndiyo maana mimi na Ngwea tumeamua kuja hapa Chuo cha Sanaa Bagamoyo ili kujiongezea maujuzi zaidi. Hata kama utakuwa juu kwenye sanaa ya muziki huwezi kujua kila kitu, itafikia kipindi lazima ujifunze,” alisema Bushoke.

Aidha, Bushoke alisema kwamba, wakiwa chuoni hapo watapiga kozi fupi ya miezi mitatu, kabla ya kutunukiwa vyeti ambavyo vitatambulika na chuo hicho.
***********************************************

Jordin Sparks: hawa ndiyo wanaume aliojirUsha nao
Mkali wa muziki wa Pop kutoka pande za Obama (Marekani), Jordin Sparks ambaye hivi sasa yuko juu kupitia ngoma kadhaa kama ‘Step At a Time na No Air aliyoigonga na Chriss Brown, ndiye staa tunayedondoka naye kupitia safu hii, ‘Ebwana Dah!’, baada ya kupata meseji za kutosha kutoka kwa wasomaji na wapenzi wa msanii huyo.

Kwa mujibu wa kale kamtandao ketu, Jordin Sparks hana listi ndefu ya mastaa wa kiume aliyowahi kujiachia nao kama ilivyokuwa kwa wasanii wengine waliyopita kunako ‘Ebwana Dah!. Mastaa wa kiume waliyowahi kula raha na binti huyo mwenye umri wa miaka 19 hivi sasa ni pamoja na Steph Jones (2004-2008), Chris Richardson (2007-2008) na Blake Lewis (2008).

Jordin Brianna Sparks ambaye ana urefu wa futi sita na macho ya rangi ya Dark Brown, huku nyota yake ikiwa ni Nge, alizaliwa Desemba 22, 1989 huko Phoenix, Arizona, Marekani. Kwa ishu zaidi kuhusu yeye mcheki kupitia www.jordinsparks.com. Wewe msomaji, unatamani kufahamu uhusiano wa zamani wa staa yupi? Tuandikie ujumbe kupitia simu 0715-110 173.
*****************************

Witness: Wasanii tuache utovu wa nidhamu
Mshindi wa tuzo ya ‘Channel O’ mwaka jana, kupitia ngoma yake yenye jina la ‘Ziro’, Witness Kaijage amesema na safu hii kwamba, anasikitishwa na tabia za utovu wa nidhamu zikiwemo kuvuta bangi, fujo na vitendo vya ngono vinavyofanywa na baadhi ya wasanii kwani zinapoteza imani kwa mashabiki na wadau wa game hiyo, cheki na Edna Katabalo kwa stori zaidi.

Msanii huyo ambaye ni miongoni mwa wasichana wachache wanaokomaa kunako game ya muziki wa Hip Hop, pia anakerwa na kitendo cha baadhi ya wasanii wa Kibongo kuigana staili, yeye anaamini kwamba msanii hakuna haja ya kuwa kama fulani ili atoke, zaidi ni kufanya kazi kwa bidii.

“Nawaomba wasanii wenzangu waachane na tabia hizo, wabadilike ili kuifanya kazi yetu ya muziki iheshimike zaidi kama kazi nyingine. Nachojua mimi ni kwamba kujituma na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ndiyo silaa kubwa ya mafanikio, kila msanii anatakiwa ajiheshimu,” alisema Witness.

Hivi sasa staa huyo aliyekuwa akiunda kundi la Wakilisha yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya ngoma yake mpya, ‘Attention Please’ ambayo itadondoka kunako vituo vya redio na televisheni mwishoni wa mwezi huu.

*****************


1 comment: