Kama nilivyoeleza wiki iliyopita kwamba, wiki hii tutaeleza jinsi ambavyo mtu unaweza kufanya Enema, ambayo ni uingizaji wa maji kupitia njia ya haja kubwa kwa lengo la kusafisha utumbo mkubwa (large intestine) na kuondoa sumu mwilini (detoxification), sasa endelea…
KUNA AINA NYINGI ZA ENEMA
Awali ya yote, unapswa kuelewa kwamba kuna aina nyingi za Enema na madhumuni yake yanatofautiana. Kuna Enema ya kidaktari anayofanyiwa mgonjwa hospitalini kwa lengo la kusafisha utumbo mpana ili kuona matatizo ya kiafya yaliyomo tumboni, kwa kitaalam inaitwa ‘Barium Enema.
Kuna Enema za kumfanyia mtu kama adhabu, ambayo hufanywa haswa na vikundi vya utesaji wa binadamu au hutumika kama njia ya kumshurutisha mtu kusema jambo bila kupenda.
Aidha, kuna kundi la watu ambao hutumia Enema kama njia moja wapo ya kuamsha hisia zao za tendo la kufanya mapenzi, ama kwa maumbilie ya kawaida au kinyume na maumbile, kitaalam wanaitwa KlismaphiliacsauKlismos.
Halikadhalika bidhaa zinazotumika kuchanganya Enema zinatofautiana, kuna wanaochanganya na dawa mbalimbali (herbals), mafuta, kahawa (Coffee Enema) na wanaotumia maji pekee, ambayo ndiyo tutakayoizungumzia leo.
UNAHITAJI NINI KUFANYA ENEMA?
a. Kitu cha kwanza kinachohitaji ili ufanye Enema ni ufahamu na malengo yake. Kama unahitaji Enema kwa ajili ya kusafisha na kulinda mwili wako, basi inapendeza ukaifanya mwenyewe au ukafanyiwa na mpenzi wako. Kila mtu anaweza kufanya Enema kwani ni kitendo ambacho hakihitaji msaada wa mtu, labda uamue kufanya hivyo.
b. unapaswa kuwa na kifaa maalumu cha kufanyia kazi hiyo, kwa kitalamu kinajulikana kana Enema Kit au Enema Bag, kifaa ambacho ni safi na salama. Muundo wa Enema kit unatofautiana, kuna zile za mfuko (Quarts) na zile za Pot, lakini zote ni sawa, inategemea utapendelea kifaa kipi.
c. Unahitaji sehemu yenye staha ambayo utaitumia ukiwa umejilaza, bila kusumbuliwa na kitu chochote. Chumbani kwako kunaweza kuwa sehemu nzuri au bafuni kama ni kusafi na kuna nafasi ya kutosha. Unahitaji kuwa na taulo za kutosha na uwe karibu na choo, kwani utakitumia kila baada ya dakika kadhaa. Pia unahitaji mafuta ya ngozi kwa ajili ya kulainishia.
No comments:
Post a Comment