Saturday, April 4, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

Dar es Salaam Hands up Temeke
Temeke ndiyo wilaya iliyokuwa imebaki, leo ndani ya shindano lako la kijanja ‘Dar es Salaam Hands Up’ (Dar es Salaam Mikono Juu) tunawadondosha mastaa wa muziki wa kizazi kipya waliotajwa kuwakilisha pande hizo baada ya kuwapata wale wa Kinondoni na Ilala wiki iliyopita.

Wasanii waliyotajwa kuiwakilisha Wilaya ya Temeke ni Stara Thomas, Juma Nature, Mh. Temba, KR, Maunda Zorro, Inspector Haroun, Dogo Mfaume, D-Knob na Chegge. Tunakushukuru wewe msomaji na mpenzi wa shindano hili kwa kutuma kura yako iliyosababisha kupatikana kwa wawakilishi wa wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni, Ilala na Temeke.
Unajua nini kitafuta wiki ijayo? Usikose kuchungulia.

Steve ‘aachana’ na Blue
Tabasamu ya kwake Henri Samir ‘Mr. Blue’ a.k.a Kabaisa ndiyo ngoma iliyomfanya atambulike zaidi na kuwa juu ile mbaya, pale aliposimama kwenye ‘korasi’ na kupiga voko za ukweli japo alikuwa na kazi yake pembeni yenye jina la ‘Nimeshindwa’, Edna Katabalo anadondoka nayo.

Namzungumzia kijana Steve kutoka pande za Zizzou Entertainment, Dar es Salaam ambaye alisema na ShowBiz kwamba, hivi sasa anaendelea kusimama kama yeye, siyo na Mr. Blue tena ili awaoneshe mashabiki wake kuwa yeye pia anaweza kuwashirikisha wasanii wengine.
“Natarajia kuachia ngoma mbili ambazo ni ‘Ulikuwa’ niliomshirikisha Datazi na ‘Baby Girl’ niliompa shavu Ngwea. Hivi sasa nipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha video zake,” alisema Steve.
Moe Q: Najuta kuzinguana na Ray C
Msanii Mohamed Chalamila a.k.a Moe Q ambaye hivi sasa anaelekea kusimama kileleni na ngoma yenye jina la ‘Thamani Yako’ amesema na ShowBiz kwamba, anajutia kitendo cha kutofautiana na dada yake, Rehema Chalamila ‘Ray C’ kitu ambacho kimemfanya asisite kumuomba msamaha.

Akipiga stori na safu hii, msanii huyo ambaye tayari ana albamu moja mtaani yenye jina la ‘Machozi’, alisema kwamba, imefikia hatua sasa yeye na dada yake, Ray C stori hazipandi kitu ambacho k kimemfanya aombe msamaha japo kosa lake halijui vizuri.

“Kitu ninachokumbuka mimi, siku moja nilimshauri ‘sista’ asijiingize kwenye ishu za vilevi kwa kuwa yeye ni msichana tena mrembo, lakini kumbe ndigu yangu hiyo ilimkera akanipigia simu na kuniwakia, kuanzia siku hiyo hataki hata kuongea na mimi,” alisema Moe Q.
Besta na Come come
Msanii Besta Prosper ambaye hana a.k.a akiwa masomoni pande za kwa Museveni (Uganda) ametuma salamu kwa mashabiki wake wa Bongo akiwaambia kwamba hajaikimbia game ya muziki kwa kuachia ngoma mpya yenye jina la ‘Come Come’.

Kazi hiyo ambayo imefanyika Uganda ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vyema hivi sasa kupitia vituo kadhaa vya redio na imetabiriwa na baadhi ya mashabiki kwamba, itamrudisha binti huyo kwenye kilele cha muziki.

Siku kadhaa zilizopita baadhi ya vyombo vya habari viliwahi kumtaja msanii huyo kuwa, amekwenda kujichimbia jijini Mwanza, baada ya kuona game linazidi kuwa gumu kwa upande wake, kitu ambacho kimeonekana ni tofauti.

1 comment:

Anonymous said...

hana lolote bora aache muzik atafute la kufanya, maana kila atoacho si muelewi kabisaaa....... au kwa ajili kaka Ruge anakinga kifuaaaa