Tollywood Kuibua vipaji vipya vya muvi
Kampuni inayokuja juu kunako ishu ya kuandaa na kusimamia filamu za Kibongo, Tollywood ya Dar es Salaam imeandaa bonge la shindano ambalo litawafanya wasanii chipukizi katika fani ya uigizaji kuwa maarufu Barani Afrika.
Mpambano huo ambao utaanza hivi karibuni kwa jina la ‘Movie Star Scouting’ utakuwa unaibua vipaji vya waigizaji hao nchi nzima na kuviendeleza kupitia filamu mbalimbali itakazokuwa inaziandaa na kuwafanya wawe mastaa kama tulivyosema hapo awali.
Msimamizi wa ishu hiyo kutoka Tollywood, Hamie Rajab, alisema na ShowBiz kwamba, shindano hilo litaishirikisha mikoa yote nchini ambapo wasanii hao wanaochipukia watatakiwa kununua fomu za ushiriki zitakazotolewa na kampuni hiyo na kuzijaza kabla ya kufanyiwa usaili.
“Washindi watakaopatikana mikoani watakuja Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki fainali kubwa ambapo washindi wawili watapata nafasi ya kuingia mkataba wa miaka miwili na Kampuni ya Tollywood ambapo watacheza filamu kadhaa zitakazowafanya walipwe shilingi milioni kumi kila mmoja.
“Kwa kuanza watashiriki katika filamu mpya, ‘Siku za Mwisho za Uhai Wangu’ ambayo pia itawashirikisha wasanii wengine maarufu kama Ray, Kanumba, Johari na Jokate. Fomu za ushiriki zitauzwa kwa shilingi 5,000 tu,” alisema Hamie Rajab.
Kampuni ya Tollywood ndiyo watengenezaji wa ‘muvi’ zilizotamba sokoni kama Fake Pastors na From China With Love. Kama wewe unadhani una kipaji cha kuigiza huu ndio wakati wako wa kuwa staa wa filamu Afrika. Kaa tayari kwa taarifa kamili.
**********
A.Y kusepa Ethiopia
Akiwa anaonekana kivingine kwenye sura yake baada ya kuibuka na miwani ya aina yake inayofanana na ile anayopenda kugonga mwana Hip Hop Kanye West wa Marekani, msanii Ambwene Yesaya ‘A.Y’ ameendelea kupata mashavu ya kutosha kutoka pande mbalimbali duniani.
Akipiga stori na ShowBiz juzi Jumatano, A.Y alisema kwamba siku chache baada ya kutoka Marekani alikopiga shoo kadhaa amepata shavu lingine nchini Ethiopia ambako atakwenda kuangusha shoo kunako tamasha kubwa lenye jina la Selam Music Festival litakalofanyika Addis Abbaba Aprili 30, mwaka huu.
********
Mamia wajitokeza kutuma kura zao
Dar es Salaam Hands Up (Dar es Salaam Mikono Juu) ndiyo jina la shindano hili la kijanja ambalo kwa kushirikiana na wewe msomaji na mpenzi wa mpambano huu linatafuta wilaya moja ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo ina wasanii wakali wa Bongo Flava.
Likiwa linaingia katika wiki ya tatu sasa tangu lilipoanza rasmi, wasomaji, wapenzi na wadau wa burudani Bongo wameonesha kulipokea kwa mikono miwili ambapo wamekuwa wakituma kura zao kwa wingi kiasi kwamba wilaya mbili zimefungana katika nafasi ya pili kitu ambacho kimetufanya tushindwe kuanza zoezi la kutoana leo.
Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam zinazowania nafasi moja ya ushindi ni Kinondoni, Ilala na Temeke. Tunatoa nafasi nyingine kwako wewe msomaji na mpenzi wa mpambano huu, endelea kutuma kura yako ukiitaja wilaya ambayo unadhani ina wasanii wakali, kisha tuma kwenda simu namba 0787-110 173. Kumbuka kwamba shindano hili linauhusu Mkoa wa Dar es Salaam na wasanii wanaoishi hapo, haijalishi kama wametoka mikoani. Kura yako ndiyo itaifanya wilaya yenye wakali wa Bongo Flava iwe juu.
**********
Nakaaya kusimama na Kikosi
Msanii aliyekula shavu la kupiga kazi na Kampuni ya Sony ya Marekani, Nakaaya Sumari ni miongoni mwa wakali wa Bongo Flava atakayesimama stejini kwa ajili ya kutoa sapoti kwa kundi la Kikosi cha Mizinga litakapokuwa linaitambulisha rasmi studio yao mpya, Kikosi Record katika Ufukwe wa Coco Beach, Jumapili ya wiki hii.
kisema na ShowBiz, kiongozi wa kundi hilo ambalo lipo kwenye mapambano makali na watu wanaodili na mauaji ya Maalbino nchini, Kalama Masoud ‘Kalapina’ a.k.a Nabii Koko alisema kwamba, mbali na Nakaaya wasanii wengine kibao wamealikwa katika ishu hiyo ya kipekee.
“Wasanii kama Mansolii, Rado, fage, Imam Abas na wengine kibao tutakuwa nao katika ‘mcharuko’ huo wa kuhakikisha studio yetu ‘Kikosi Record’ inazinduliwa kwa amani,” alisema Kalapina.
********
Frank Wasanii hawapendi kukosolewa
Kutoka ndani ya game ya maigizo ShowBiz ilikutana uso kwa uso na msanii Mohamed Mwikongi a.k.a Frank ambaye alikiri kwamba, wasanii wengi, hasa waliopo kunako mradi huo hawapendi kukosolewa ndiyo sababu inayowafanya wachemke katika kazi zao, Chile Kasoga anashuka nayo.
Ndani ya safu hii Frank alisema kwamba, inapotokea msanii akamkosoa msanii mwenzake kwa nia ya kuboresha anaweza akasababisha uhasama mkubwa baina yao. “Unajua filamu zetu zina makosa mengi ikiwemo baadhi ya wasanii kushindwa kuonesha uwezo katika filamu wanazoigiza lakini ukijaribu kuwakosoa unaweza kuvunja hata urafiki uliokuwepo kwa muda mrefu,” alisema msanii huyo.

*****
No comments:
Post a Comment