Tuesday, April 7, 2009

JE, UMEWAHI KUFANYA ENEMA?- 4


KAma tulikuwa pamoja katika makala tatu mfululizo zilizopita, kwa kusoma makala haya ya nne na ya mwisho, utakuwa umeelewa kwa kina maana ya Enema na jinsi ya kuifanya. Hii ni njia ya asili ya kusafisha tumbo ambayo imekuwepo tangu enzi za mabibi zetu na wale ambao wameizingatia kwa kujisafisha matumbo yao mara kwa mara, wamenufaika sana kwa kuwa na afya njema na kuwa huru na maradhi mbali mbali.

Nimekuwa nikipata maswali mengi kutoka kwa wasomaji wetu kuhusu mada hii, wengi wamedhani Enema ni kama dawa ya kunywa au kutumia, wakati hiki ni kitendo tu cha kusafisha mwili wako kwa kutumia kifaa maalum pamoja na maji masafi na wala hakina madhara yoyote kwa mfanyaji, endelea..

MAANDALIZI

a.Utahitaji maji safi na salama ya uvugu uvugu, ya ujazo wa kati ya lita 3 na 5, kutegemeana na uwezo wako wa kuhimili kiasi cha maji tumboni. Ili usipatwe na maumivu ya tumbo yasiyo ya lazima, maji yasiwe ya baridi sana wala ya moto sana.

b.Tayarisha kifaa chako kwa kuchomeka mrija wake sehemu yake. Funga koki yake, tia maji kisha kiweke sehemu yenye muinuko kutoka sehemu uliyolala ama kining’inize umbali wa mita moja au mbili kutoka mahali ulipolala, ili maji yaweze kutiririka vizuri.

c.Lala ubavu, kisha andaa sehemu zako za nyuma kwa kulainisha kwa mafuta ya ngozi halafu ingiza taratibu mrija wa maji na ufungue bomba taratibu huku ukisikilizia maji yanavyotembea tumboni. Kitendo hiki hakina maumivu ya aina yoyote na hukamilika kwa muda usiozidi dakika 10.

Unapaswa kufungua maji taratibu na udhibiti mwenendo wake kwa kushikilia koki yake, unapohisi tumbo kuuma, funga koki na shusha pumzi huku ukipapasa tumbo lako taratibu, kisha endelea tena kuachia maji taratibu.

Wakati ukifanya zoezi hilo, utakuwa ukihisi kwenda haja, jaribu kujizuia kwa kiwango utakachoweza, ukifikia kiwango chako cha mwisho cha kujizuia, funga koki yako kisha chomoa mpira kutoka kwenye koki ambayo utaizuia kwenye makalio ili itumike kama kizuizi chako.

Jaribu kujizuia japo kwa dakika 3 mpaka 10 kisha nenda chooni ukiwa na koki yako kweye makalio. Ufikapo chooni ondoa koki na maji yote yatatoka kwa kasi yakiambatana na kinyesi na uchafu mwingine, utajisikia umeshusha mzigo mzito na kujisikia mwepesi sana! Fanya zoezi hilo kwa wakati huo mara mbili mpaka tatu, kulingana na utakavyoweza.

Ili ufanikiwe kuondoa uchafu mwingi tumboni, ukiwemo ule ulioganda kwa miaka mingi na kuwa kama tope (mucus), inashauriwa zoezi hilo lifanyike angalau kwa siku tatu mfululizo.

Kwa watu wenye nafasi, Enema wameifanya kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku, hivyo huifanya kila wiki au mwezi. Lakini kwa watu wasio na nafasi hiyo, inashauriwa kuifanya japo mara moja kwa mwaka na faida zake ni nyingi sana, ambazo tutazieleza siku zijazo.

ENEMA HUFANYIKA WAKATI GANI

Unaweza kuifanya Enema wakati wowote. Wakati mzuri zaidi ni muda mfupi kabla hujaenda kulala. Unaweza kuifanya baada ya chakula chako cha jioni, mchana au asubuhi. Zoezi hili haliwezi kuingiliana na chakula utakachokuwa umekula muda mfupi kabla ya kufanya Enema.

MWISHO.

1 comment:

Anonymous said...

mjomba naona hiyo dawa inaweza kuwasababisha watu kuwa machoko baadae