Ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa burudani wa mjini Bukoba imewadia, ni keshokutwa yaani Jumapili ya Pasaka ambapo msanii Rutta Maximilian Bushoke kutoka Zizzou Entertainment akiwa na msafara wa mastaa kibao wa muziki wa Bongo Flava wataangusha bonge la shoo pande hizo.
Ndani ya ShowBiz Bushoke alisema kwamba, kila kitu kuhusu shoo hiyo ya utambulisho wa albamu yake, Dunia njia’ kimekamilika na muda mchache kuanzia sasa msafara wa kuelekea Bukoba utakuwa njia moja ukizingatia kwamba wasanii wote watakaosafiri naye wapo katika afya nzuri.
“Shoo ya kwanza tutapiga ndani ya Ukumbi wa Linas Pub kwa kiingilio cha shilingi elfu kumi kwa kila mtu, siku itakayofuata, yaani Jumatatu ya Pasaka tutaangusha muziki ndani ya Uwanja wa Kaitaba kwa kiingilio cha buku moja tu. Katika msafara huo nitakuwa na wasanii kama Mwasiti, Blue, Maunda Zorro, Ngwea, Steve na wengine kibao,” alisema Bushoke.
*********************************************



Shindano lako la kijanja, ‘Dar es Salaam Hands Up’ (Dar es Salaam Mikono Juu) leo limeanza rasmi kwa kuwaleta kwako wasanii wote wanaoziwakilisha wilaya zao, yaani Ilala, Temeke na Kinondoni ili wewe msomaii na mpenzi wa mpambano huu, hususasi mdau wa burudani Bongo utuambie ni wilaya ipi ina wasanii wakali.
Unachotakiwa kufanya ni kuwacheki kwa makini mastaa hao wanaoziwakilisha wilaya zao, kisha andike ujumbe mfupi (SMS) katika simu yako ya kiganjani ukiitaja wilaya ambayo unadhani inastahili kuibuka na ushindi. (mfano ILALA, kisha tuma kwenda simu namba 0787-110 173).
Kumbuka kwamba, wewe msomaji na mpenzi wa burudani nchini ndiyo jaji wa shindano hili. Baada ya kupokea kura zetu kwa wiki mbili mfululizo tutaanza zoezi la kutoana mpaka atakapopatikana mshindi mmoja. habari ndiyo hiyo msomaji, kazi kwako.
************************************

Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliyokuwepo kwenye shoo ya mchizi kutoka pande za Marekani, Chingy Howard Bailey iliyofanyika ndani ya Viwanja vya Leades Club, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita walisema na ShowBiz kwamba, msanii huyo ni wa kawaida sana stejini.
Ndani ya safu hii msanii Ambwene Yesaya ‘A.Y’ ndiyo alikuwa wa kwanza kutamka kwamba. “Shoo ya Chingy haikuwa ya ukweli sana tofauti na watu wengi walivyotegemea, ni msanii wa kawaida tu, binafsi naamini kwamba, miaka kadhaa ijayo wasanii wengi wa nje hasa Marekani na Ulaya kwa ujumla watakuwa hawana nafasi kubwa Bongo kama ilivyokuwa siku za nyuma”.
kwa upande wake Mohamed Mbwana ‘MB Dog’ ambaye ni mwanamuziki bora wa kume 2008/09 alisema kuwa. “Yaani huwezi amini, wasanii wa Bongo wamepiga shoo kali zaidi kuliko Chingy, nadhani we mwenyewe ulishuhudia mashabiki walivyokuwa wanaruka na shoo zetu tofauti na alivyopanda mchizi, mwanzo mashabiki walishangilia lakini kadri muda ulivyozidi kwenda walionekana kuchoka,”.
2 comments:
kigezo gani kilichotumika hadi T.I.D hasiwepo kinondoni
FID Q anaiwakilisha MWANZO sio KINO na NGWEA anawakilisha East ZOO DODOMA mbona mnachemka.
AU MSHAPANGA MATOKEO
Post a Comment