
Ebwana Dah! Yaani jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, ndivyo ilivyo kwa mkali wa michano mwenye maskani yake pande za Marekani, Lil Wayne ambaye kwa mujibu wa mtandao ameshajiachia na mademu saba, kitu ambacho mashabiki wengi walikuwa hawakifahamu.
Kabla sijashuka chini zaidi, kama wewe ni shabiki wa Wayne nakufahamisha kwamba, pichani juu chini ya Lil Wayne ndiye ‘kifaa’ chake, Teairra Mari ndiyo jina lake na ni msanii wa muziki wa R&B ambaye walianza kujiachia naye tangu mwishoni mwa mwaka jana.
Tukirudi nyuma kidogo, Lil Wayne alianza kujirusha na mwanadada Farrah Franklin kabla hajahamishia majeshi kwa mdogo wake Beyonce, Solange Knowles, kisha akadondokea kwa mwana R&B Nivea mwaka 2003 hadi 2004.
Baada ya kutoka kwa Nivea, Wayne alidondokea kwa mrembo Antonia Carter ambaye alifanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja wa kike kabla hawajapigana chini mwaka 2006. Mwana Hip Hop wa kike, Trina ndiye lilikuwa chaguo lingine la Lil Wayne baada ya kuachana na mzazi mwenzie huyo, lakini ndoto za kuishi pamoja kama mke na mume ziliyayuka 2007 ambapo wawili hao walitosana kiaina.
Mwisho wa siku mwana Hip Hop huyo mwenye mafanikio ya kutosha alijikuta akiangukia kwa binti mwenye mvuto wa kipekee, Sarah Bellew kabla ya kumshiti na kudondokea kwa mwanamuziki Teairra Mari. Kwa wale ambao walitutumia ujumbe wakitaka kufahamu Lil Wayne amewahi kujiachia na mastaa wa kike wangapi nadhani watakuwa wametusoma vizuri. Wewe pia kama unapenda kufahamu uhusiano wa zamani na sasa wa staa yeyote wa Kiwanja tutumie ujumbe mfupi kupitia simu namba 0787-110 173.
No comments:
Post a Comment