Baada ya kulumbana kwa siku kadhaa msanii aliyejiajiri kupitia game ya muziki wa kizazi kipya Mohamedi Chalamila ‘Moe Q’ ameamua kuinua mikono kwa Ray C na kuufunga mjadala huo kwa kusema kwamba, kama staa huyo ambaye ni dada yake wa damu ameamua kumkana hana budi kuachana naye na kuendelea na maisha yake kama alivyoshauriwa na ndugu zake wengine akiwemo baba yao mdogo, Rhobi Chacha alipiga naye stori.
Moe Q, ambaye hivi sasa ana ‘bang’ hewani na ngoma yake yenye jina la ‘Thamani yako’ alisema kwamba, ameamua kuachana na malumbano hayo kwa sababu Ray C alimpigia simu baba yao mdogo na kutishia kumpeleka yeye polisi kwa kuwa amekuwa akimchafua kupitia baadhi ya vyombo vya habari.
“Kama yeye siyo ndugu yangu kwanini alimpigia simu baba yetu mdogo kuwa anataka kwenda kunishitaki polisi? Siyo kama naogopa kwenda polisi bali nimeamua kuachana naye baada ya wazee kunishauri. Huko polisi yeye ndiyo angeumbuka na naamini ipo siku tutakutana kwenye matatizo hasa ya kifamilia, ikiwemo misiba,” alisema Moe.
Msanii huyo tayari ana albamu moja mkononi yenye jina la ‘Machozi’ yenye ngoma kibao zikiwemo ‘Thamani yako’, ‘Emi’, ‘Dodoma’, ‘Namtafuta’, ‘Zawadi’, ‘Life Goes on’ na Unapotoka. Wasanii aliyowapa shavu ni pamoja na Q-Chiller, Ngwea, Bwana Misosi, Yakuza Mobb, Zerlo K na Bashary Cassim.

3 comments:
WENZENU majuu wanaanzisha beefs ili wavute watu in the process wanaunda mkwanja,sasa nie na njaa zenu mabeef mpaka kwenye vyombo vya habari what for
Duh!! Kwani ni kipi cha kupigania? Kuwa ndugu tu? Mara nyingi ndugu hugombea mirathi, na kama hakuna la kugombea basi waendelee na shughuli zao na watakutana kutakakowakutanisha
Crazy ppl baada ya kuchukulia bahati ya vipaji kama baraka na kuungana na kutoa album pamoja mnagombana for what? Statement yenyewe iliyotolewa haina hata maana kama watoto vile eti kasema kwa baba mdogo this and that??? so?
Post a Comment