Aileen - 'stering' wa filamu ya From China With Luv
Tollywood movies Itakufanya staa wa Afrika
Je, wewe ni msanii unaechipukia kunako sanaa ya filamu Bongo? Kama uko poa Kampuni nya Tollywood ya Dar es Salaam imeandaa bonge la shindano kwa ajili yako, ambalo litakufanya uwe staa wa Afrika na kuondoka na mkwanja usiopungua shilingi milioni kumi.
Msimamizi wa shindano hilo kutoka Tollywood, Hamie Rajab amesema na ShowBiz kwamba, mpambano huo utakwenda kwa jina la ‘Movie Star Scouting’ na kwamba utaihusisha mikoa yote Tanzania ambapo washindi wawili watakaopatikana kila sehemu watakutana kwenye fainali kubwa zitakazofanyika Dar es Saalam.
“Washiriki wote watatakiwa kununua fomu za ushiriki na kuzijaza, kisha watafanyiwa usahili ambapo washindi wawili watakaopatikana kila mkoa watapata nafasi kushiriki kwenye fainali kubwa zitakazofanyika Dar es Salaam. Washindi wawili, msichana na mvulana watakaopatikana kwenye fainali hizo watapata nafasi ya kuingia mkataba wa miaka miwili na Kampuni ya Tollywood.
“Mkataba huo utawawezesha kucheza filamu kadhaa zitakazowafanya walipwe shilingi milioni kumi kila mmoja. Kwa kuanza watashiriki kwenye sinema mpya, ‘Siku za Mwisho za Uhai Wangu’ ambayo pia itawashirikisha mastaa wengine kama Ray, Kanumba, Johari na Jokate. Fomu za ushiriki zitauzwa kwa shilingi 5,000 tu,” alisema Hamie Rajab.
Kampuni ya Tollywood ndiyo watayarishaji wa filamu zinazotamba sokoni kama Fake Pastors na From China With Love. Kama wewe unadhani una kipaji cha kuigiza huu ndiyo wakati wako wa kuwa staa wa filamu Afrika. Kaa tayari kwa taarifa kamili.
**********

TMK Family walibipu jeshi
Kundi la muziki wa kizazi kipya, TMK Wanaume Family linatarajia kudondosha video ya wimbo wao mpya, ‘Wanaume Kazini’ siku chache zijazo huku ndani yake wasanii hao wakionekana kupiga gwanda za jeshi kitu kinachotafsiriwa kama ni ‘kulibipu’ jeshi la wananchi ambalo lilipiga marufuku mavazi hayo kwa raia.
ShowBiz ambayo ilifanikiwa kuicheki video hiyo na kumuuliza meneja wa kundi hilo, Said Fella imekuaje wakatumia nguo za jeshi ambazo zilipigwa marufuku? “TMK Wanaume Family kama kundi la wasanii hatuoni kama ni kosa kutumia nguo za aina hiyo kwenye video, tunachojua sisi ukivaa nguo za aina hiyo na kutembea mitaani ndiyo kosa.
Aidha kwa upande mwingine Fella alisema kwamba, wakiwa na kombati hizo za kijeshi wamefanikiwa kufanya video ambayo inaweza kuwa bora kuliko zote za muziki wa Bongo Flava zilizotangulia kutoka. Video hiyo ambayo imefanyika kupitia Kampuni ya Visual Lab chini ya mtayarishaji Adam Juma inatoka ili kuitambulisha albamu ya kundi iliyopewa jina hilo hilo, ‘Wanaume Kazini’.
Kwa upande mwingine, Said Fella naye amefanikiwa kukamilisha albamu yake yenye jina la ‘Mkubwa na wanawe’, huku msanii wake, Amani James ‘Mh. Temba’ naye akijiandaa kudondosha ya kwake yenye jina la ‘Mtoto wa kichaga’ ambayo inatambulishwa na nyimbo kama Maneno Yawachoma, Kiulaini na nyingine kibao.
*******
Dar es Salaam Hands up: Ilala yafunga pazia
Haya tena kumekucha, shindano lako la kijanja, Dar es Salaam Hands Up (Dar es Salaam Mikono Juu) limeanza kupamba moto. Baada ya kupokea kura nyingi kutoka kwa wasomaji na wapenzi wa mpambano huu kwa takribani wiki kadhaa leo tunaitaja wilaya moja ambayo inatoka.
Kwa mujibu wa meseji kibao zilizotumwa na wasomaji ambao ndiyo majaji, tunachukua fursa hii kuitaja Wilaya ya Ilala kuwa ndiyo inafungua pazia la kutolewa kwenye mpambano huu baada ya kuambulia kura chache ikiziacha Temeke na Kinondoni zikichuana vikali.
Msomaji, kumbuka kwamba shindano hili linaitafuta wilaya moja kati ya tatu zilizopo katika Mkoa wa Dar es Salaam ambayo ina wasanii wakali wanaofanya muziki wa kizazi kipya. Baada ya kukumbusha hilo tunaomba uendelee kutuma kura yako ukiitaja wilaya ambayo unadhani ina wasanii wakali kati ya Kinondoni na Temeke zinazoendelea kupambana.
Zoezi la kutuma kura yako liko vile vile, andika ujumbe mfupi (SMS) ukiitaja wilaya hiyo kisha tuma kwenda simu namba 0787-110 173. Tunarudia kukumbusha kuwa, shindano hili linauhusu Mkoa wa Dar es Salaam na wasanii wanaoishi hapo, haijalishi kama wametoka mikoani.
********
No comments:
Post a Comment