Monday, May 4, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!



Tollywood Kutoa shavu kwa wasanii wa maigizo
Shindano jipya na la kisasa ‘Movie Star Scouting’ ambalo litatafuta vipaji vya waigizaji chipukizi lililoandaliwa na Kampuni ya Tollywood ya Dar es Salaam, linatarajia kuanza hivi karibuni kwa kusambaza fomu katika mikoa yote ya Tanzania ambazo zitawawezesha wasanii hao kupata nafasi ya kushiriki.

Kwa mujibu wa msimamizi wa mpambano huo kutoka Tollywood, Hamie Rajab kila kitu kuhusu ishu hiyo kimeshakamilika, kinachosubiriwa ni siku maalum ya kusambaza fomu hizo ambazo zitauzwa kwa shilingi 5,000 kila mmoja na kuwawezesha washiriki wote nchini kuingia kwenye mchujo wa kwanza, kabla ya kufanyika kwa fainali kubwa jijini Dar es Salaam.

“Washiriki wote watatakiwa kununua fomu za ushiriki na kuzijaza, kisha watafanyiwa usahili ambapo washindi wawili watakaopatikana kila mkoa watakuja Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki kwenye fainali kubwa. Washindi wawili, msichana na mvulana watakaopatikana kwenye fainali hizo watapata nafasi ya kuingia mkataba wa miaka miwili na Kampuni ya Tollywood,” alisema Hamie Rajab.

Aidha, msimamizi huyo alisema kwamba, mkataba huo utawawezesha washindi hao kucheza filamu kadhaa zitakazoandaliwa na Kampuni ya Tollywood na kuwafaya walipwe shilingi milioni 10 kila mmoja ambapo kwa kuanza watashiriki kwenye muvi mpya, ‘Siku za Mwisho za Uhai Wangu’ ambayo pia itawashirikisha mastaa wengine kama Ray, Kanumba, Johari na Jokate. Je, wewe ni mmoja wa wasaniii ambao una ndoto za kuwa kama mastaa hao na kujulikana Afrika nzima? Huu ndiyo wakati wako.

Kampuni ya Tollywood ndiyo watayarishaji wa filamu zinazotamba kama Fake Pastors na From China With Love.
****************************
Paris hilton
Avunja rekodi ya safu hii, miaka 28 wanaume zaidi ya 65!
Ebwana Dah! Hii ya leo kiboko, inawezekana staa wa mitindo, filamu na muziki, Paris Hilton kutoka pande za Marekani akawa amevunja rekodi ya safu hii kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa wa kiume zaidi ya 65, kitu ambacho hakijawahi kutokea tangu tulipoanzisha kona hii.

Wale wasomaji wengi wa safu hii walioomba kufahamu staa huyo wa kike amewahi kujiachia na wanaume wangapi leo wanaweza wasiamini macho yao, zaidi ya kushangazwa na msururu mrefu wa midume hiyo ya Paris Hilton. Kwa mujibu wa mtandao unaodili na ishu hizo, mastaa hao wa kiume ni Jared Leto, Randy Spelling (1995 - 1997) na Stavros Merjos (1999).

Wengine ni Edward Furlong (1999 -2000), Oscar De La Hoya (2000), Leonardo DiCaprio (2000) Rick Salomon (2000) Ajay Popoff (2000) Brandon Davis (2001), Elijah Blue (2001), Nick Lachey (2001), Tom Sizemore (2001), Jason Shaw ( 2001 - 2003), Vincent Gallo (2002), Val Kilmer (2002 ñ 2006) na Mark McGrath (2003).
Mwanadada huyo hakuishia hapo, aliendelea kujirusha na mastaa wengine wa kiume kama Nicolas Cage (2003), Carlo Mondavi (2003), Ingrid Casares (2003), Deryck Whibley (2003),

Brian Urlacher (2003), Jamie Kennedy (2003 - 2005), Rob Mills (2003 - 2004), Nicole Lenz (2003), Nick Carter (2003 - 2004), Brian Quintana (2004), Joe Francis (2004), Lucas Bain (2004), Robert Evans (2004), Chad Muska (2004) na Jake Sumner (2004 - 2005).

Msururu huo uliendelea kwa Chad Murray (2004), Simon Rex (2004), Fred Durst (2004), Mark Philippoussis (2004), Paris Latsis (2004 - 2007), Colin Farrell (2004 ñ 2005), Stavros Niarchos III (2005 ñ 2007), Erik MacArthur (2005), Matt Leinart (2005 - 2006), Kevin Pietersen (2005), Jack Osbourne (2005 - 2006), Aaron Carter (2006), Adam Levine (2006), Mario Lopez (2006), Jose Theodore (2006) na Travis Barker (2006 ñ 2008).

Baada ya hao, Paris aliendelea kula raha na Criss Angel (2006), Andy Roddick (2006), Joel Moore (2007), Josh Henderson (2007), James Blunt (2007), Hunter Cross (2007), Tyler Atkins (2007), Alex Vaggo (2007), Adrian Grenier (2007), Julian Feitsma (2007 - 2008), Chris Dewolfe (2008), Brody Jenner (2008), Elisha Cuthbert (2008), Benji Madden (2008) na Doug Reinhardt wa mwaka huu wa 2009.

Akiwa na umri wa miaka 28 sasa, Paris Whitney Hilton ana urefu wa futi tano na nchi sita, alizaliwa Februari 17, 1981 pande za New York City, Marekani. Ukitaka kumcheki zaidi chungulia kwenye website yake, www.parishilton.com.

No comments: