Wednesday, May 20, 2009

MITANDAO JAMII NA UHURU WAKO

Kama wewe ni mtembeleaji wa mitandao sana haswa kama unatafuta marafiki au kama unataka kukutana na watu mbali mbali umeshakisikia kitu kinaitwa SOCIAL NETWORKS – MITANDAO JAMII hii ni mitandao unayoweza kukutana na watu mbali mbali au jamii za watu mbali waliokuwa na sifa ambazo wewe unazihitaji wa kutoka sehemu mbali mbali duniani wengine huwa wanaweka picha zao na mambo kama hayo

Miaka 10 iliyopita watu wengi walikuwa wanatafuta marafiki wa mtandao epals wengine wanaita penpals kwa kutembelea tovuti maalumu ambazo watu walikuwa wanajiandikisha kwa ajili ya huduma hii wengine walikuwa wanalipia huduma hii , ila kwa miaka ya sasa kuna tovuti nyingi sana zimekuja ambazo zimeziba kabisa nafasi ya mitandao ya kirafiki hiyo ya penpals au inayofanana na hiyo

Kwa sasa huduma ya MITANDAO JAMII ndio iko juu zaidi moja ya mitandao hii mikubwa ni FACEBOOK tembelea www.facebook.com ukijiunga na facebook unaweza kutafuta marafiki wengi sana na unaweza kuwasiliana nao wakati wowote unapotaka hata kwa kutumia simu yako ya mkononi yenye huduma ya mtandao , unaweza kubadilishana picha na mambo mengine mengi sana hata unaweza kuchat ( bonga ) na mtu papo kwa hapo

Watu wengi haswa wa nchi za magharibi wanatumia mtandao huu kwa ajili ya kupashana habari nyingi sana haswa watalii ambao wanasafiri sehemu mbali mbali duniani , hata mashiriki makubwa ya kijasusi na kipelelezi yanatumia sana mitandao hii kwa ajili ya kupata taarifa za baadhi ya watu na mienendo yao kwa karibu zaidi .

Pia mitandao hii inaingizia sana mapato serikali ambapo mitandao hii imesajiliwa kwa sababu kampuni nyingi sana zinatumia mitandao hii kwa wingi kutangaza bidhaa zao na taarifa zingine zaidi ya tovuti kama yahoo au hotmail kwa sasa mitandao jamii inakuja juu sana haswa hiyo facebook

Mfano ukiingia katika www.facebook.com andika neno Fisadi Dagaa , majibu yatakuja kama kweli kama kuna mtu mwenye jina hilo pamoja na maelezo yake mengine ya ziada zaidi utaweza kuona rafiki zake wengine anaowasiliana nao kwenye mtandao huo au ambao amewahi kuwasiliana nao ingawa ni ngumu kujua mtu huyo anawasiliana kutokea wapi kutokana na wengine kujisajili na taarifa za uwongo .

………………………………………………………………………………………………………………………

SUALA LA USALAMA WAKO

Unapojiunga katika mitandao hiyo mingi huwa inatuma mialiko ( invitation ) kwenda katika anuani zako zote kama ni yahoo au gmail au hata hotmail bila idhini yako wewe , hii inaanisha kama mtu akipata mwaliko ule na kuwezi kujiunga atakuwa rafiki yako na ataweza kuona unawasiliana na wakina nani zaidi .

Wengine huwa wanaweka picha zao katika mitandao hii , mitandao hii haina sheria kali kuhusu picha zinazohifadhiwa mule hata kama ni za uwongo kama sio za matusi basi zinaachwa zikae hapo hapo , wengine huwa wanachukuwa picha katika tovuti hizo nakwenda kuzitumia katika maeneo mengine ya kazi zao au za kidhalilishaji zaidi

Mfano katika mtandao wa zeutamu kuna wanafunzi wengi sana wa IFM walikuwa wanapeleka picha kule ambapo zilitolewa facebook na hi5 au tagged wakaziedit kidogo kisha kuzituma zeutamu kwa faida zao wenyewe , wengi picha hizi wanazitumia katika magezeti na vijarida vyao bila idhini ya mfano facebook au hi5 hili ni suala la kisheria zaidi mimi sio mtaalamu wa sheria hata hivyo .

Kwa kuwa mitandao hii inavutia sana vijana wahalifu hutumia sana mitandao hii kwa ajili ya shuguli zao za kutafuta watu wa kuwasaidia kufanya uhalifu wao sehemu mbali mbali duniani , mfano unaona picha ya msichana mrembo sana katika mtandao , wewe unafikiria kuwasiliana nae ndio utawasiliana nae haswa walio nchi za mbali anaweza kukuomba umtumie pesa ili aweze kuja hapo ulipo wewe, ukishatuma pesa ndio unaweza usimwone tena na mawasiliano yakatike unakuta kuna watu zaidi ya alfu 2 wameona picha hiyo na wamependa kuwasiliana nae ( unaweza kuhisi anatengeneza pesa kiasi gani mtu huyo ?)

Wengine wanaona picha hizo haswa za wasichana walio katika nchi masikini wanawaahidi ajira nchi za ngambo wakienda kule ni kuuzwa kwenye madanguro pamoja na sehemu zingine za anasa utashangaa mbona ndugu yako harudi nyumbani wala hawasiliani kwanini ??

Hayo ndio mambo yaliyo katika mtandao jamii hii ingawa kuna wengine wanafanikiwa kufaidika sana na mitandao hii kwa kupata watu waaminifu wa kuwasiliana nao hata wengine kuowana na kufanya biashara ila wengi zaidi ndio wahanga wa matukio mengi ya kihalifu yanayoendeshwa kwa njia ya mtandao

Kwahiyo kijana mwenzangu unapotumia mitandao hii uwe makini sana kama hujui uliza upate uzoefu wa wenzako wanafanyaje kuweza kuhimili vishindo hivi vipya vya mitandao usiingie kichwa kichwa

Mwisho kama nilivyosema hapo juu mashirika mengi ya kijasusi na kipepelezi yanatumia mitandao hii kusaka wahalifu hata kutafuta wafanyakazi wapya basi hata hapa Tanzania vyombo vyetu vya usalama viwe makini sana katika kufuatilia mitandao hii pamoja na wanachama wake kwa faida zao na wengin.

YONA MARO – FOR BIDII AFRIKA YA MASHARIKI

No comments: