Tuesday, June 23, 2009

BINADAMU HATUKUUMBWA TUUGUE - 2


Inaendelea kutoka wiki iliyopita

You are what you eat
UTAKAPOUGUA UFANYE NINI?
Naweza kusema kuwa tatizo kubwa tulilonalo ambalo linatusumbua ni kutokujua jinsi ya kutibu miili yetu pale tunapopatwa na tatizo la kiafya. Katika suala la ugonjwa, kabla ya kupata tiba, chanzo cha ugonjwa lazima kieleweke. Mazingira machafu yabadilishwe, ulaji usio sahihi uachwe kisha mwili usadiwe kujisafisha wenyewe kwa kuondoa sumu mwilini kwa kutumia dawa zisizo na madhara zikisaidiwa kwa kiasi kikubwa na vyakula sahihi.

Unapopatwa na ugonjwa ikiwa ni matokeo ya ukiukwaji wa zile kanuni za mwili, swali la kwanza kujiuliza ni nini kimesababisha ugonjwa huo, kwa sababu hakuna ugonjwa usiokuwa na sababu. Jiulize; ‘nimefanya nini mpaka nimeugua’? Mwanzoni swali hilo linaweza kuwa gumu na usipate jibu, lakini ukizoea na ukiwa makini na vitu unavyokula kila siku, jibu hupatikana kirahisi.

Baada ya kujua nini kimesababisha ugonjwa wako, ondoa sababau hiyo na acha kula au kufanya jambo hilo kisha anza kujitibu kwa kutumia dawa asilia ambazo zitakusaidia kuondoa sumu iliyoko mwilini na bila kukuletea madhara mengine. Jambo la kuzingatia hapa ni kuepuka matumizi ya dawa zenye sumu kutibu ugonjwa ulionao, kwani badala ya kutibu unaweza kuwa unajiongezea maradhi mengine zaidi.
Baada ya kuelezea kwa kirefu kanuni za mwili, tuangalie vitu muhimu anavyopaswa kuvitumia binadamu kila siku bila kukosa kutokana na umuhimu wake katika kufikia lengo la kuwa na afya bora:

MAJI
Sumu hurundikana mwilini tunapokuwa hatuna maji ya kutosha mwilini. Kitoto kichanga kilichozaliwa leo, asilimia 80 ya mwili wake ni maji. Kiwango cha maji kwenye tishu hupungua kadri mwili unavyoongezeka hadi kufikia asilimia 60 kwa mtu mzima.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, binadamu aneweza kuishi hadi siku 81 bila kula, lakini hufa anapokosa maji kwa muda wa siku 5 tu! Mtu anapopoteza asilimia 5 ya maji mwilini, hubadilika na hueza kuanza kuweweseka, misuli kushikana na kukosa mwelekeo na akipoteza maji kwa asilimia hadi 15 maisha yake huwa hatarini na kupoteza maji kwa aziaid ya silimi 15 mtu hufa.
SABABU 9 KWA NINI UNYWE MAJI
Kupunguza uzito: Kunywa maji mengi kunasaidia kupunguza uzito, kwani maji hayana mafuta, kalori wala sukari.

Afya ya moyo: Unywaji wa maji mengi kunaweza kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo. Utafiti wa miaka sita uliofanywa Marekani umeonesha kuwa watu wanaokunywa glasi za maji zisizopungua 5 kwa siku, hujiepusha na uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo kwa asilimia 41 zaidi ya wale wanaokunywa glasi 2 au chini ya hapo.

Nishati ya mwili: Mwili unapopungikiwa maji, hukufanya ujisikie mchovu, hivyo kwa kunywa maji ya kutosha daima utakuwa mwenye nguvu. Pendelea kunywa maji badala ya vinywaji baridi kama soda, juisi au bia.

Tiba ya kichwa: Dalili ya mtu kupungukiwa maji mwilini ni pamoja na kuumwa kichwa. Kunywa maji ya kutosha na hutasumbuliwa sana na kuumwa kichwa mara kwa mara.

Ngozi nyororo: Unywaji maji ya kutosha kila siku unaweza safisha ngozi yako na kuifanya ionekane nyororo.

Matatizo ya choo: Maji ni dawa ya kutibu ukosefu wa choo, kunywa maji ya kutosha kila siku na utajiepusha na tatizo la ukosefu wa choo mara kwa mara.

Usafishaji wa mwili: Maji husaidia kuondoa sumu mwilini kwa kutoa uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa.

Saratarani: Utajiepusha na saratani ya tumbo kwa kunywa maji, kwani maji husaidia suala la usagaji wa chakula tumboni na hivyo wakati wote tumbo lako litakuwa safi. Utajiondoa katika hatari ya kupata saratani ya tumbo kwa asilimia 45 na asilimia 50 kwa saratani ya kibofu cha mkojo.

Mazoezi: Mwili unapokuwa na maji ya kutosha, yatakufanya uwe na nguvu ya kufanya mazoezi yako ya kutosha, hivyo kupata faida ya mazoezi ipasavyo.

JALI AFYA YAKO...

5 comments:

Anonymous said...

Habari kaka Mrisho! Naomba ushauri wako mwanangu ana mwaka na nusu yaani swala la maji huwa ni shida mpk tunakabana na atayatapika sijui kwa nini hapendi maji juisi ya machungwa aaa mwake je asipokunywa maji kwa siku akapewa hiyo juisi hata glasi 2 hapo vp?Maana msichana wa kazi cjui kama anamkaba kumpa maji.

Anonymous said...

Habari ya leo! tatizo langu nisipokunywa chai kichwa kinauma vibaya mno mpk inabidi ninywe badala ya kupata dawa na ningependa zaidi niache chai nitumie soya ila hilo ndio tatizo na chai nasikia ni sumu ukiizoea ulishawai kuzungumza kuhusu chai ila hukutamka sumu ni watu nasikia wakisema je lina ukweli?

Mrisho's Photography said...

juice siyo maji, hata ukinywa juice bado unahitaji kunywa maji kwa ajili ya digestion ya hiyo juice _ wanatuambia wataalamu. Hivyo nakushauri mkazanie sana mwanao kuzoe kunywa maji, tumia mbinu ya kumuwekea maji mengi kwenye juisi, baada ya muda atazoea kunywa maji. suala la maji halina mjadala dada, lazimamwisho wa siku anywe maji tu.

kuhusu kuumwa kichwa unapokunywa chai, hiyo imetokana na kuuzowesha mwili hivyo na sasa umekuwa addicted, kama vile teja la unga. Nakushauri jaribu water therapy kwa muda flani pengine tatizo la kuumwa kichwa linaweza kuisha. kunywa maji mengi asubuhi kabla kula chochote (lita moja hadi moja na nusu ukiweza) then baada ya hapo fungua kinywa na utakacho, ukienda nayo hiyo therapy kwa muda wa wiki 2 hadi 4, hatausipokunywa chai kichwa kinaweza kisiume.

Ila, water therapy inapoanza kufanyakazi mwilini (kuondoa sumu mwilini) kihcwa huuma kwa muda, hivyo usishangae pia, ni kawaida na baada sumu kuisha au kupungua huwezi kusikia kichwa kikiuma hata ukinywa maji mengi kiasi gani.

KWA MAELEZO ZAIDI KUHUSU WATER THERAPY, CLICK LINK YAKE HAPO (chini ya asante kwa kunisoma hapa) KULIA USOME MAKALA ZILIZOPITA

Anonymous said...

Mrisho, pole na kazi. Ninashukuru sana kwa ELIMU YAKO YA AFYA ZETU. Muda wa nyumba ulileta hii habari kuhusu kunywa maji (30min-1hr)kabla ya breakfast, na maji yawe ya vuguvugu.

Mimi nilikuwa nasumbuliwa sana na kupata haja kubwa, pia na kuumwa kichwa. Baada ya kuanza kufanya kama ulivyoeelekeza yaani najisikia kama nimezaliwa upya, kichwa hakiumi tena, tumbo jepesi na mini najisikia mwepesi.

Tatizo langu halikuwa kwamba nilikuwa sinywi maji, maji ndiyo kinywaji changu kikubwa cha kila siku (2-3 ltr daily). Ila nilikuwa nakosea tu. Nilikuwa nakunywa maji baada ya kula, tena ya baridi kupita kiasi.

Mwanzoni nilipata tatizo la kunywa maji mengi kwa mara moja tena ya vuguvu,lakini sasa hivi imekuwa routine na NAWASHAURI WENGINE WAJARIBU.

Anonymous said...

Nakukubali dr mrisho mtu zake sifa kupewa mungu akuzidishie uzidi kutufahamisha hayo unayoyajua si utani uwa nafarajika na kujifunza mengi kupitia glob yako peace