2Face (Nigeria) - Mshindi Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa R&B
D'Banj (Nigeria) - Mshindi Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Mwaka
M.I (Nigeria) - Mshindi Tuzo za Mwanamuziki Bora wa Hip Hop na Chipukizi
P-Square: (Nigeria)- Washindi Tuzo ya Kundi Bora
AY (Tanzania); akilakiwa na mashabiki wake wakati akipita Red Carpet..alizidiwa na M.I
Sara 'Shaa'(Tanzania)...aliwania tuzo ya Mwanamuziki Bora Chipukizi, akazidiwa na M.I
Nameless (Kenya) .. (kulia) alijinyakulia tuzo mbili, Mwanamuzii Bora wa Kiume na Chaguo la Msikilizaji..akiwa pamoja na AY na Seven wa MTV Tanzania.

Kwanini Nigeria tu?
Je, ni kweli tuzo za MTV Africa ni za Nigeria tu? Kwanini kila mwaka wanapata tuzo nyingi? Bila shaka hilo ni swali linaloulizwa na wapenzi wengi wa muziki na wafuatiliaji wa tuzo hizo kwa sasa ambazo mwaka huu zilifanyika Nairobi nchini Kenya, ambako AY na Shaa walituwakilisha, showbiz ina data kamili.
NIGERIA INAJIVUNIA NINI?
Katika Bara la Afrika, Nigeria ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi, hadi sensa ya hivi karibuni, Nigeria ilikuwa na jumla ya watu milioni 146, idadi ambayo ni zaidi ya mara tatu ya watu wa Tanzania na ni zaidi ya watu wote wa Afrika Mashariki: Tanzania (milioni 40), Kenya (milioni 38) na Uganda (milioni 28)!
Mbali ya kuwa na watu wengi, lakini ni ukweli uliowazi kuwa Nigeria ina wasanii wengi na wa fani mbalimbali. Kwa mantiki hiyo nchi nyingine za Kiafrika haziko katika nafasi nzuri ya kushinda dhidi ya Nigeria linapokuja suala kama hili la tuzo.
Kila mwaka tumeshuhudia wasanii wapya wakiibuka kwa kishindo. Kwa Bongo, 2Face alikuwa wa kwanza kujulikana na kutamba, wakafuatia P-square, kisha amekuja D’Banj ambaye kwa mwaka wa pili mfululizo anajitwalia tuzo ya mwanamuziki Bora wa Mwaka na hadi huko Uingereza amebatizwa jina la ‘Koko Master’. D’BanJ ni wa siku nyingi nchini kwao.
Ikiwa ndiyo kwanza D’banj anatamba Bongo kiasi cha kuwafunika wenzake waliomtangulia kujulikana, msanii mwingine anayejulikana kwa jin la M.I tayari ameibuka na kuanza kujulikana kimataifa na kujinyakulia tuzo mbili ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki. Ni msanii mpya lakini ni hatari.
SIRI YA USHINDI WA NIGERIA
Mbali ya kuona ukweli kwamba Nigeria ina idadi kubwa ya watu na wasanii wengi, lakini siri nyingine ya ushindi wao, hasa katika mashindano yanayotumia njia ya kura kumpata mshindi, ni idadi ya watu wanaojitokeza kupiga kura, iwe kwa mtandao ama simu.
Kwa kuwa wao wapo wengi, linapokuja suala la kupiga simu au kura kwa njia yoyote ile, wao wana nafasi nzuri ya kumpa kura nyingi wamtakaye. Lakini pia, wenzetu wana muamko mkubwa katika masuala ya matumizi ya teknolojia ya mawasiliano, ukilinganisha na nchi za Afrika Mashariki na Kati.
NINI KIFANYIKE
Jambo pekee linaloweza kufanyika ili kuboresha tuzo hizi, ni waandaaji kubadili utaratibu wa sasa na kuweka utaratibu mwingine wa kuwapata washindi, ikiwa ni pamoja na kuweka category za kushindaniwa na wasanii wa eneo au nchi moja.
Sisi tunaamini kuwa tuzo hizi hazina upendeleo wa aina yoyote na wala haziwezi kuwa zilianzishwa kwa ajili ya maslahi ya Nigeria au Afrika Kusini pekee, bali ni kwa Afrika nzima kama bara lenye vipaji lukuki.

1 comment:
wa nigeria wako juu sana tu tusiwabebe wanamuziki wetu tukubali tu kwa sasa tukaze buti kwa sana tu
Post a Comment