Friday, March 19, 2010

IJUMAA SHOWBIZ


Fid Q "Bi Kidude hanifahamu japo nimepiga naye kazi”
Ngosha The Don a.k.a Fid Q amedondosha kali ya mwaka, kupitia ShowBiz amesema kwamba, wimbo wenye jina la Juhudi za wasiojiweza aliyompa shavu Bi. Kidude alichukua takribani mwaka mzima kuurekodi.

“Kikwazo alikuwa ni Bi. Kidude ambaye tulikuwa tunapishana kila ninapomfuata Zanzibar. Siku tuliyofanikiwa kufanya kazi hiyo nilipanda ndege hadi Zenji lakini pamoja na kufika mapema nilifanikiwa kumpata usiku, tukaingia ndani ya studio za Jupter, tukapiga kazi.

“Pamoja na kukaa na Bi. Kidude studio kwa saa kadhaa, kesho yake nilipokutana naye na kumsalimia akawa amenisahau, akaniuliza we nani? Sikumshangaa sana kwakuwa ameenda eji kimtindo!!!” alisema Fid.

Ngoma hiyo ya Fid na nyingine kibao zinapatikana ndani ya albamu yake yenye jina la Propaganda.
**************************************************************

Mnyalu I love U na mwanaye live
ShowBiz ambayo iko juu kukuletea wewe msomaji michongo inayoendelea kwenye game ya burudani, leo imeidaka ishu mpya kutoka kwa Mike Mwakatundu a.k.a Mnyalu ambaye kitambo kirefu alipotea kwenye mradi wa muziki.

Akiwa ni mwajiriwa wa kampuni moja ya simu za mkononi Bongo, Mnyalu amerudi kivingine akisikika na ngoma yenye jina la I Love U, huku uvumi ukiwa umeenea kitaani kwamba alipotea kwenye sanaa coz alikuwa bize akimsaidia waifu wake kumlea mtoto wao, Mike Junior (pichani).
************************************************

*************************************************************

ArnoldSchwarzenegger
The Big Boss wa jimbo kubwa la Carfornia huko kwa mzee Obama, Arnold Schwarzenegger ambaye pia ni mkali wa muvi za kibabe anatarajia kuingia rasmi mzigoni mwezi ujao kurekodi mwendelezo wa filamu za kutisha, Terminator.

Mshua huyo wa muvi ya ‘Commando’ mwenye umri wa miaka 61 sasa atarekodi vipande vya Terminator siku tano za mwanzo wa mwezi ujao, kisha kurudi kuendelea na majukumu ya kiserikali kabla ya kurejea tena kufanya shughuli hiyo majuma matano baadaye.

Kazi ya kukamilisha mpango mzima wa Terminator 4 inatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka ujao na ishu nzima ikipangwa kutumia mzigo wa dolla milioni 90 hadi 100.
************************************************************

Werrason atikisa Paris
Mchizi anayeendelea kufunika kunako game ya muziki wa Soukouss na kiongozi wa kundi la ‘Wenge Musica Maison Mere’ Noel Ngiama Makanda a.k.a Werrason amefanikiwa kuingiza jina lake kwenye vitabu vya kumbukumbu, baada ya kupiga shoo kubwa kupitia tamasha lililotikisa mji mkuu wa Ufaransa, Paris siku chache zilizopita.

Tamasha hilo lililokwenda kwa jina la Zenith lilikusanya zaidi ya mashabiki 800 waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo pande za Uingereza walionunua tiketi zao kupitia mtandao wa Werrason aliyewahi kutikisa dunia kupitia ngoma ya ‘Kalayi Boying.’
Compiled by mc george/ijumaa newspaper

No comments: