Monday, June 14, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ

Zuhura Vipaji vyake vinamtesa
Kutoka katika game ya muziki wa kizazi kipya msanii Zuhura Mrisho a.k.a Zuhura ambaye pia anashikilia taji la Nokia Face of Africa 2006, lililomjumuisha kwenye ramani za mastaa wa Bongo, amesema na Abby Cool & MC George Over the Weekend kuwa anahangaishwa sana na vipaji alivyonavyo kiasi kwamba anashindwa kuelewa atumikie kipi.

Akipiga stori na safu hii juzi ndani ya Studio za 24/7 zilizopo Mikocheni Dar alipokuwa anarekodi ngoma mpya, Historia chini ya mtayarishaji muziki, Villy, Zuhura alisema. “Mh! Nachoka mwenzenu, Zuhura unayemuona hapa ni mwanamuziki, muigizaji, mwandishi wa mashairi, halafu pia ni fundi rangi za magari na nyumba, ukinikuta nimekula ovaroli langu nimeshika kopo la rangi utakoma mwenyewe.”

Akiwa anafanya vyema hivi sasa kupitia ngoma yenye jina la Shida na raha aliyompa shavu Banana Zorro, mrembo huyo aliyepitia nyuma ya vipaji, THT alitambulishwa kwenye game ya muziki kupitia wimbo wenye jina la Limupenzi, mpaka sasa anamiliki albamu moja kitaani yenye jina hilo hilo.
**************************

Bongo Fleva: Nyimbo kali, video mh! inakuwaje?
Bado tupo katika harakati za kuutetea muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva kwa kuangalia ishu mbalimbali zinazoweza kusababisha game hii ikaelekea kaburini kama dalili zinavyoonesha hivi sasa.

Ishu ya msingi hapa siyo bifu na wadau wa sanaa hiyo isipokuwa sisi kama wadau wa burudani tunataka mwisho tujenge na kuufanya muziki wetu urudi juu kama zamani. Kuna haka kamchezo, ambako sijui kameanzia wapi jamani...ujue nini? Wasanii wa Bongo Fleva bado wanajitahidi kugonga ngoma nzuri, lakini linapokuja suala la video, mh! Ni aibu.

Wapo baadhi ya wasanii wanazitendea haki video za nyimbo zao, lakini wapo pia wanaozinyima haki, sijui ni kwasababu ya kukurupuka ili kuwahi kuonekana kideoni au bajeti. Lakini kama ni bajeti mbona wanafanya video na makampuni makubwa kwa gaharama za juu, vipi washindwe kuzitendea haki. Tunachotaka kusema hapa ni kwamba, utashangaa kuona wimbo mkali ambao ndani ya video yake unastahili kuingizwa shoo za nguvu, msanii anaonekana kaganda sehemu moja akibadilisha pozi za hapa na pale na kuonesha pamba za thamani.

Matokeo yake ukiiangalia kazi hiyo utahisi hakuna tofauti kati ya audio ya kusikiliza na video, kwasababu wasanii hawachezi zaidi ya kutingisha miguu na kutembea ufukweni! Acheni kulipua bwana, igeni mifano ya wenzenu, angalieni video za mbele muone masela anavyojipanga....mfano mzuri ni Makhrikhiri, ona wanavyojaza watu kila wanapopiga shoo, unajua kwasababu ya nini? Ndani ya video zao mashabiki wamependa zaidi shoo, ukizingatia kwamba wanaimba kawaida tu. Siyo uchawi. Onesheni manjonjo kwenye video kwa kuweka shoo za ukweli kama nyimbo zenu zilivyo! Hadi next week.
***********************


Ciara Awachanganya 50 Cent, Ludacris
Ebwana Dah! Kama kawa ipo on air ikijiachia kiana na leo inakuletea kwa uchache kuhusu wanaume waliowahi kula maraha na mwanamuziki Ciara Harris a.k.a Ciara.

Stori iliyoshushwa na mtandao unaodili na ishu za nani kajiachia na nani huko majuu, inamtaja moja kwa moja kinda wa Muziki wa Hip Hop, Bow Wow kama ndiye mwanaume wa kwanza kuripotiwa kula malavedave na Ciara. Bow Wow alijiachia na Ciara kwa kipindi cha mwaka mmoja, kuanzia 2005-2006 alipojiweka pembani kwasababu ambazo hazikutajwa, unaona bwana!

Baada ya hapo Ciara aliingia kwenye likizo ya mapenzi kwa kipindi cha mwaka mmoja, kabla hajakutana na 50 Cent ambaye alitanua naye kwa miaka miwili, yaani 2007 - 2009. Pamoja na kwamba haikujatajwa sababu za Ciara kutemana na 50 Cent, lakini habari za chini chini zinaeleza kwamba, usaliti ndiyo sababu kubwa inayotajwa kuwatenganisha, kwani baadaye ilijulikana kwamba, wakati Ciara akila bata na black American huyo alikuwa akijiachia kwa kujiiba na Ludacris ambapo baadaye ikawa siyo siri tena kwani walikuwa wakionekana viwanja mbalimbali na kuifanya idadi ya mastaa aliyojiachia nao kufikia watatu.

Jina lake halisi ni Ciara Harris a.k.a The First Lady of Crunk au Princess of Crunk & B, alizaliwa Oktoba 25, 1985 huko Austin, Texas, ana elimu ya juu zaidi (Advanced Level) aliyohitimu Riverdale High School, mwaka 2003 huko Marekani.
*************************
compiled by mc george/ijumaa wikienda

No comments: