Friday, July 2, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Shaa: “Sasa naweza kuisaidia familia”
Staa wa ngoma ya Shoga, Sara Kaisi a.k.a Shaa amefunguka na kuweka wazi kwamba, hivi sasa anaweza kuisaidia familia yake wakiwemo wazazi kwakuwa tayari ameshaanza kuchungulia mafanikio kupitia game ya muziki wa kizazi kipya.

Akiongea kupitia kituo cha redio Clouds FM cha Dar es Salaam juzi kati, Shaa alisema kwamba sanaa ya muziki ambayo aliinza tangu 2004 hivi sasa imemfanya aishi vizuri huku akiisaidia familia yake kwa mambo mbalimbali ikiwemo kuleta misosi mezani.

“Huko nyuma wakati naanza muziki sikuwa na uwezo wowote, lakini sasa naweza kuwasaidia hata wazazi wangu,” alisema Shaa ambaye hivi sasa anafanya vizuri na kupitia kazi hiyo, Shoga ambayo tayari inaonekana kupitia vituo kadhaa vya luning baada ya kufanyiwa video.

*******************************************
MB Dog: Aacha simanzi Bongo!
Akiwa bado anaendelea kuwarusha wakazi wa Uingereza kwa ngoma zake za kitambo kama Latifah, Siuliniambia, na nyingine zilizomfanya wamvute pande hizo, msanii Mohamed Mbwana a.k.a MB Dog ameanza simanzi Bongo kupitia ngom yake mpya yenye jin la ‘Kilio changu’.

ShowBiz ambayo imepata bahati ya kuitegea sikio kazi hiyo ambayo hivi sasa ipo hewani kupitia vituo kadhaa vya redio ilimsikia msanii huyo akilalamika kwa sana hali iliyomfanya ashindwe kuendelea kuimba na kumuacha prodyuza akipiga vinanda mpaka mwisho wa ngoma.

Akipiga stori na safu hii kwa njia ya mtandao kutoka pande za Uingereza, Dog alisema kwamba kitu kilichomfanya adondoshe chozi wakati akirekodi ngoma hiyo ni stori ya ukweli iliyomkuta katika safari yake ya muziki ambayo alikuwa anaizungumzia ndani ya kazi hiyo.

“Kaka nilishindwa kuendelea kuimba, inauma sana, unafanya kazi nzuri ambazo zinakubalika na watu wengi lakini hupati kitu zaidi ya kuendelea kuwa maskini,”alisema Dog ambaye anatarajia kupiga kambi Uingereza kwa takribani wiki tatu.
******************************************
Wyfil Davi: Miaka 30 yampeleka resi
Kwa mara ya kwanza Bongo na ndani ya game ya muziki wa kizazi kipya huu ndiyo unaweza kuwa mkataba wa kwanza mrefu kufanyika kati ya mwana Bongo Flava na meneja wake, ambao umewashitua watu wengi huku wengine wakidhani ni zuga tu.

Ukweli ni kwamba kijana mpya ndani ya mradi wa muziki huo, Wilfred David a.k.a Wyfil Davi yuko resi na kazi ili kuhakikisha mkataba wa miaka thelathini aliyosaini na meneja wake, Ustaadhi Juma unakuwa wa mafanikio ya kutosha.

Akipiga stori na safu hii juzi kati msanii huyo alisema kwamba kupitia mkataba huo tayari ameshagonga kazi mbili, ‘Ninong’oneze’ na Nina kasoro gani aliyosimama na mwanadada Rehema Chalamila a.k.a Ray C zote zikiwa tayari zimefanyiwa video. “Bado natamani kufanya kazi na wasanii wengi wakubwa akiwemo Chid Benz ili kufika kimataifa zaidi”.

*************************************************
KalaJeremiah: Asepa Kampala, apagawa na demu wa Kiganda
Ishu mpya iliyodondoka ndani ya ShowBiz kutoka pande za Kampala, Uganda zinasema kwamba, mwana Hip Hop Kala Jeremiah amesepa Bongo hivi karibuni na kutua nchini humo baada ya kukolea kwa demu wa Kiganda (pichani) ambaye jina lake halikuweza kupatikana fasta.

Kwa mujibu wa mdau mmoja wa safu hii aliyopo pande hizo na ambaye hakupenda jina lake tulichore hapa, Kala anaonesha kukolea kwa mrembo huyo kiasi kwamba haoneshi nia ya kurudi Bongo hivi karubuni.

“Jamaa kila unapomuona yuko ‘veri krozi’ na demu wake, iwe klabu, beach na sehemu nyingine ‘touni,” alisema mdau huyo ambaye kila alipokuwa anamfanyia taimingi staa huyo wa Bongo Flava kwa ajili ya kumgonga maswali alikuwa anaambulia bilabila.

Kala ambaye ni zao la shindano la Bongo Star Search na aliyewahi kufanya vyema na ngoma kama ‘Tanzania’, ‘Ushamjua’ na nyingine anadaiwa kudondokea pande hizo miezi kadhaa iliyopita kitu ilichoacha maswali kwa baadhi ya mashabiki wa muziki wake wakihoji staa huyo yuko wapi.

ShowBiz inakuahidi kwamba, itaendelea kumfuatilia msanii huyo ili kujua mengi zaidi kuhusu demu huyo na kama ndiyo aliyesababisha yeye akatoweka Bongo ghafla, kisha itaweka kila kitu kweupe. Endelea kucheki na sisi.

Compiled by mc george/ijumaa newspaper

No comments: