Monday, July 12, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Mona Weee, mimi niliwe denda? Watasubiri sana!
Black beauty mwenye swagger za kiduu, Yvonne-Cherry Ngatikwa a.k.a Monalisa ameeleza kilichomo ndani yake na kufunua kwamba tangu aanze kuvuma kwenye Kiwanda cha Filamu Bongo zaidi ya miaka 10 iliyopita, hajawahi kuliwa denda on shooting.

Mona, aliiambia Abby Cool & MC George over the weekend kuwa ingawa amekuwa akionesha uhalisia hata kwenye zile scene zinazomuonesha akiwa deep in malavi davi, lakini hajawahi kumpa ulimi wake msanii wa kiume hata mmoja aliyecheza naye ki-baba na mama.

Alisema, kama itaonekana kwenye kioo akiwa amenoga kimahaba, basi kuna ‘maujanja saplai’ yanayofanywa na watayarishaji ili kunogesha ‘mzigo’, lakini hata mara moja hajawahi kuthubutu.

“Busu la ulimi (denda) ni kitu cha thamani sana siwezi kutoa kwa kila mtu, kwani kuna watu wengine huwa siyo wasafi vinywani mwao licha ya ustaa walionao,” alisema Mona akijibu swali la paparazi wa safu hii, Hemed Kisanda.
********************
Amber Rose: Kutemwa na Kanye, chanzo ni kumegeka nje!
Yamesemwa mengi kuhusu mdada Amber Rose kupigwa chini na mchizi aliyempa jina, Kanye West! Imezungumzwa kuwa staa wa Jesus Walk aliamua kumshit mwanamitindo huyo kwa sababu ni binti mapepe!

Ebwana Dah! Inakuja na jibu kamili kuwa the Hip Hop Legend, Kanye, amempiga chini Amber baada ya kubainika kwamba ameanza kumegeka nje kwa staa wa Rugby, Reggie Bush.

Site ya kiwanja ambayo inavuma kwa flagi la kuanika uhusiano wa mastaa mbalimbali Mtoni, inaliweka jina Reggie kuwa ndiye jamaa anayekamata malavi davi ya mwanamitindo huyo kwa sasa. Hata hivyo, site hiyo inabaki na majina mawili tu ya wanaume kwamba ndiyo waliowahi kujikunja na Amber! Kanye kuanzia mwaka 2008 hadi 2010 kisha Reggie ambaye amedaka mchuma hii 2010 mpaka nukta hii.

Kwa upande wa Reggie ambaye anazidiwa miaka miwili na Amber, anafunuliwa kuwa kabla ya kutua kwa mwanamitindo huyo, alijiweka kwa mrembo Kim Kardashian kati ya 2007 na 2010. Amber, alizaliwa Oktoba 21, 1982, Philadelphia, Pennsylvania, Marekani. Umri wake ni miaka 27. Reggie yeye jina lake kamili ni Reginald Alfred Bush II, alianza kugongwa jua Machi Pili, 1985, Spring Valley, California, Marekani. *************************

Magali Azichana filamu Bongo, aanika ufyatu wa wasanii kugonga malavi davi ya ukweli Behind the Scene!
Galacha wa Kiwanda cha Filamu Bongo, Charles Tobias Magali, amezichana muvi za Bongo na moja kwa moja amewaendea hewani waigizaji na kuwaumbua kuwa wana mchezo wa kufanya kweli behind the scen!

Staa huyo ambaye hutambulika zaidi kama Mzee Magali, alikunjuka wiki iliyopita kuwa waigizaji wengi hukosa nidhamu ya kusikiliza maagizo ya directors, hivyo kuanza kufanya yao ambayo hayaendani na maadili ya sanaa.

“Muongozaji anasema hivi wao wanafanya vile, hili ni tatizo kubwa wakati wa kurekodi. Nyingine ni pale wanapokutana wasanii ambao wana uhusiano wa kimapenzi na kupangwa scene moja, ni balaa!

“Ni kweli kabisa watu wanashikana na kutomasana sana nyuma ya kamera. Wakati mwingine ni kwa ‘Masihara’, ingawa wapo wengine ambao hukumbwa na mfadhaiko inapotokea wamecheza kipande cha kulala kitandani,” alisema Mzee Magali. Imegongwa na Na Hemed Kisanda.
**************************
Q-Chiller aitosa taarabu
Super Musician mwenye sauti ya kubembeleza, Aboubakar Shaaban Katwila ‘Q-Chiller’ yupo kimya, watu wakadai kaishiwa, lakini ikavumishwa kwamba jamaa kaamua kugeukia mtindo wa Mwambao a.k.a Taarab, baada ya yote hayo, Abby Cool & MC George over the weekend imefanikiwa ku-capture neno lake mwenyewe.

One on One talk between Q-Chiller na safu hii, inaweka hadharani kuwa staa huyo hana mpango na Taarab, isipokuwa kuna mambo ya msingi ambayo anarekebisha. “Sina mpango wa kuimba Taarab, nipo kimya kwa sababu kuna vitu binafsi naweka sawa,” alisema Q-Chiller 10 days ago na kuongeza:

“Unajua ukitaka kufanya mambo mazuri hutakiwi kuyatangaza mpaka yatakapokuwa tayari, kwahiyo siku nikikamilisha nitawajulisha mashabiki wangu na ninaamini watafurahi.” Imegongwa na Na Gladness Mallya. ********************************
Jaffarai: Afya yatengemaa, punde atarudi barabarani
Icon wa Bongo Hip Hop, Jaffari Ally Mshamu ‘Jaffarai’ ana-recover kwa kasi, anachofanya kwa sasa ni kufuata maagizo ya madaktari wake ambao wamemtaka apumzike kwa kipindi cha mwezi mmoja kabla ya kurudi barabarani.

Akishusaha neno lake kwa mashabiki wake na Watanzania kwa jumla kwa through cellular wiki iliyopita, Jaffarai alisema kuwa anamshukuru Mungu anaendelea vizuri, ingawa kwa sasa hatakiwi kufanya chochote zaidi ya kupumzika.

“Sitakiwi kutembea wala kuendesha gari, labda niendeshwe. Natakiwa kupumzika kwanza. Nina wiki tatu mbele za kutojishughulisha na chochote halafu baada ya hapo itakuwa safi,” alisema Jaffarai na kuongeza:

“Jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba nimeshonwa nyuzi ambazo zinaozea ndani kwa ndani, siyo zile za kutoa. Nawashukuru Watanzania kwa kuniombea, nawapenda sana kwa sababu natambua thamani yao.”
*******************
Kanumba akichoka anakwenda kupumzika Sauz
Ni kali ila inaonesha sura ya mafanikio! Yamkini Kiwanda cha Filamu Bongo kinalipa, kwani ishu iliyodondoka hapa ni kuwa staa wa muvi Afrika, Steven Charles Kanumba kwa sasa kwenda Sauz, hangoji kujichaanga, ni suala la kuamua tu kama vile paparazzi kuzama kumbi za burudani.

Inafunuliwa kuwa kwa sasa Kanumba akijisikia kuchoka, anabadili upepo kwa kwenda kutembea nchi mbalimbali na hivi karibuni alitimkia Sauz ambako kulikuwa kumekucha na Kombe la Dunia ambalo tamati yake ilikuwa jana kwenye Uwanja wa Soccer City, Johannesburg, ambako Uholanzi walimenyana na Hispania katika mchezo wa fainali. Katikati ya wiki iliyopita, Abby Cool & MC George over the weekend ilifanya kumuendea hewani ili kumpa hi, lakini mchizi akaispraiz:

“Aah, kaka unakuwa mwandishi wa kwanza kuzungumza na mimi. Nimerudi jana, nilikuwa nje ya nchi.” Alipoulizwa alikuwa wapi na kwa shughuli gani, Kanumba a.k.a The Great, alijibu: “Nilikwenda Sauz kidogo. Hakukuwa na ishu special, ila kupumzika tu kidogo, nilihisi kuchoka.”

compiled by mc george/ijumaa wikienda

No comments: