Friday, August 6, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Lil' Kim

Jipangusee!! RRaaaaa!!
Lil - Kim, Bracket na ‘Aladji’ Leaders hapatoshi kesho
Baada ya shoo za mikoani, sasa ni zamu ya jiji kubwa kuliko yote, Dar ambapo Fiesta 2010 ‘Jipanguse Rrararaaaa’, itapoteza vilivyo ndani ya Viwanja vya Leaders Kinondoni kesho ikipambwa na wanamuziki wa kimataifa, Kimberly Denis Jones ‘Lil Kim’ kutoka Marekani, Bracket na Ramatulaye ‘Aladji’ kutoka Nigeria.

Stori kutoka kwa waratibu wa event hiyo, Prime Time Promotions zinaweka kweupe kwamba watanzania, kwa mara ya kwanza watapata nafasi ya kuwashuhudia wasanii hao waki-perform live kwenye jukwaa moja.

Taarifa hizo zinaeleza kwamba, hakuna mpenda burudani atakayekuwa na muda wa kukaa chini kwani burudani itakuwa ni non-stop mpaka kucheee!

Kuhusu viingilio ni buku kumi (10,000/) tu kabla ya event kuanza na buku kumi na tano (15,000) mlangoni.

Wasanii kibao Bongo nao watapata nafasi ya kuonesha shoo za ukweli. Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Mwasiti, Dully Sykes, Barnabas, Linah, Fid Q wengine wengi.

******************************************
Fally Ipupa amnasa Keri Hilson
BAADA ya kupata mafaniko kwenye ngoma ya Chaise electrique aliyomshirikisha First Lady wa zamani wa G-Unit, Olivia Longott, staa wa Soukouss kutoka pande za Congo DR, Francois Ipupa Nsimba ‘Fally Ipupa de Caprio’, ameweka kweupe mpango wake wa kugonga ngoma na mkali wa R&B huko mtoni, Keri Hilson.

Fally aliuambia mtandao wa Congo Planet.com kuwa, alikutana na Keri kwa mara ya kwanza mwezi jana huko Afrika Kusini alipokuwa akifanya shoo maalum ya Kombe la Dunia na kuzungumza naye juu ya kugonga ‘kolabo’ ambapo walikubaliana.

“Nilikutana naye Afrika Kusini wakati wa fainali za WOZA, aliniambia anapenda kazi zangu hasa ile niliyofanya na Olivia, sikusita nikamuomba tufanye kazi ya pamoja akakubali hivyo baadaye mwezi huu tutakuwa pamoja Paris, Ufaransa tukikamilisha hilo,” alisema Fally.
***********************************************************

Five Stars wamtamani Hammer Q
Siku chache baada ya kuliacha kundi la Dar Modern Taarab, staa wa muziki wa mwambao, Hussein Mohammedi ‘Hammer Q, amedaiwa kuwindwa na Kundi la Five Stars Modern Taarab.

Imedaiwa kuwa, lengo hasa la Five Stars kutaka kumchukua Hammer Q ni kuiimarisha bendi yao wakiamini kuwa msanii huyo ni kifaa.
Akiongea na safu hii, Mkurugenzi wa Five Stars, Khamis Slim aliithibitishia kuwepo kwa mpango huo na kueleza kuwa, hizo ni harakati za kuziba pengo lililoachwa na Khadija Yusuf.

“Ni kweli tunamhitaji Hammer Q ili kuimarisha kikosi chetu na huyu ni mwimbaji mzuri, kila mpenzi wa taarab anafahamu hilo ndiyo maana tunataka kuitumia nafasi hii kumnyakuwa,” alisema Slim.
******************************************************
Diamond Musica: kupiga zote kali ndani ya Mango Garden leo
Bendi ‘baba lao’ ya muziki wa dansi Bongo, Diamond Musica International ‘Vijana Classic’, leo (Ijumaa) itashusha burudani ya aina yake ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni Dar ikiwa ni sehemu ya kutambulisha nyimbo na staili zao mpya.

Akistorisha na Ijumaa Showbiz jijini Dar juzi, Kiongozi wa bendi hiyo, Mule Mule FBI aliweka plain kwamba, shoo hiyo ni maalum kwa mashabiki wao na kwamba burudani itakayoporomoshwa na vijana wake itasuuza roho ya kila atakayehudhuria.

“Itakuwa ni shoo ya nguvu ambayo kila mpenzi wa muziki wa dansi hastahili kukosa.Tutapiga nyimbo zetu mpya kama vile Power Twenty Ten, Kovu la mapenzi na supu ya kongoro sambamba na staili zetu mpya,” alisema FBI.

compiled by mc george/ijumaa newspaper

No comments: