Friday, September 24, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Chuchu Hans Ajifungia ndani saa 24
Nyota wa filamu kiwango ya ‘Roho Sita’ iliyowahi kutikisa Jiji la Bongo, kitambo kidogo kilichopita, Chuchu Hans amesema hivi sasa anaishi maisha ya kutokuonekana mtaani kutokana na kutumia muda mwingi akiwa kajifungia ndani akimuuguza mama yake mzazi anayesumbuliwa na vidonda vya tumbo, Hemed Kisanda alipiga naye stori.

Akizungunza na Ijumaa, Chuchu ambaye siku chache zijazo ataanza kuonekana tena kwenye ulimwengu wa filamu baada ya kushiriki kwenye muvi ya ‘Candle in the wind’ iliyotayarishwa na Kampuni ya Manhatan Production, aliweka wazi kuwa imemlazimu kutumia muda wake mwingi akiwa karibu na mama yake ili kumfariji na kumsaidia kwa kila anachokihataji kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa huo.

“Nampenda sana mama yangu hivyo siwezi kumuacha peke yake katika kipindi kama hiki, niko karibu naye na nina jitahidi kumhudumia kwa kila linalowezekana ndiyo maana hivi sasa sionekani kabisa mtaaani,” alisema Chuchu.

//////////////////////////////////

Will Smith Family: Waonyesha maajabu kwa vipaji, kuzunguka dunia
Nyota wa filamu nchini Marekani, Willard Christopher ‘Will Smith, Jr’ anatarajia kuanza ziara ya kuzunguka nchi mbalimbali duniani akiwa na familia yake kwa ajili ya kukusanya pesa za mfuko maalum wa kusaidia maafa ya kimbunga na mafuriko yaliyolizikumba nchi kadhaa za bara la Asia.

Kwa mujibu wa habari kutoka Miami yaliko maskani ya familia hiyo iliyojaaliwa vipaji kibao zinasema ziara hizo zitaanzia pembe ya kaskazini ya Afrika mapema mwezi Novemba na baadaye kwenye mabara mengine, kabla ya kumalizia huko Asia.

Miongoni mwa watu watakaokuwemo kwenye msafara huo ni pamoja na mke wa nyota huyo ambaye pia ni muigizaji mahiri wa filamu, Jada Pinkett, mtoto wa kwanza wa Willy aitwaye Willard Christopher Smith III, ambaye ni muigizaji na mwanamitindo, Jaden Christopher Syre aliyeigiza filamu ya Karate Kid na Willow Camille Reign ambaye hivi karibuni alisaini mkataba na kampuni kubwa ya Muziki ya Roc National inayomilikiwa na Shawn Carter ‘Jay Z.’

////////////////////////////////////

Kid Bwoy Ahamishiwa ICU!
Kutoka pande za Rock City (Mwanza), mtayarishaji muziki aliyekumbwa na balaa la kuumizwa na mtu asiyejulikana akiwa ndani ya studio yake na kulazwa katika Hospitali ya Bugando, Sandu George Mpanda a.k.a Kid Bwoy amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’.

Akipiga stori na kipindi cha Michano Time kinachorushwa na Kituo cha Radio Passion FM cha Mwanza, chini ya mtangazaji wake Phillbert Kabago katikati ya wiki hii, baba mdogo wa Kid Bwoy, Jose Mpanda alisema kwamba mgonjwa wao amehamishiwa ICU ili kumpa muda mzuri wa kupumzika tofauti na alipokuwa kwenye wodi ya kawaida.

“Napenda kuwatoa wasiwasi ndugu, jamaa na marafiki wa Kid Bwoy kwamba mgonjwa wetu anaendelea vizuri, lakini madaktari wamelazimika kumuhamishia kule kwasababu ya kumpa muda mzuri wa kupumzika. Unajua aliopokuwa amelazwa wodini watu wengi walikuwa wakija kumuona huku wengine wakitumia muda mrefu zaidi kitu ambacho kilikuwa kikimfanya apate muda mchache wa kupumzika,” alisema Jose.

Baba mdogo huyo wa Kid pia alisema kwamba, pamoja na mgonjwa wao kujitambua na kuanza kuongea, wameombwa na dokta anayemshughulikia wasimuulize maswali mengi hasa kuhusiana na tukio zima hadi pale afya yake itakapotengemaa zaidi. Kid alikumbwa na mkasa huo Jumatano ya wiki iliyopita saa 2 usiku akiwa ndani ya studio yake yenye jina la Tetemesha Records. ShowBz inampa pole za kutosha, inaendelea kumuombea apone haraka ili arudi katika hali yake na kulisukuma gurudumu la muziki wa Bongo Flava.

///////////////////////////////////

Diamond Musica Warejea tena stejini
Wakali wa miondoko ya ‘Bodaboda’ Diamond Musica International ‘Vijana Classic,’ kesho wanatarajiwa kurejea jukwaani kuonesha vitu vyao baada ya mapumziko ya wiki moja ya kuomboleza msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wao Msaidizi marehemu, Perfect Kagisa a.k.a P Diddy aliyefariki ghafla Septemba 7, mwaka huu kwa tatizo la shinikizo la damu. George Kayala anashuka nayo.

Mkurugenzi Mkuu wa bendi hiyo, Judith Moshi alisema jana jijini Dar kuwa, leo (Ijumaa) watapiga ndani ya Ukumbi wa Meeda Club – Sinza, na kesho watapagawisha Viwanja vya Leaders huku Jumapili wakionesha uwezo wao wa kucheza na kuimba pande za The River Between Mbezi.

“Baada ya kumpumzika kwa muda wa wiki moja tukiomboleza msiba wa P Diddy, kesho (leo) kama kawaida tutakuwa ndani ya Ukumbi wa Meeda, Sinza, Jumamosi tutapiga Viwanja vya Leaders na Jumapili tutapagawisha pande za The River Between Mbezi,” alisema Judith.
///////////////////////


Top 20 Bamiza, ZINAZOTESA Magic FM 92.9
1. Mama ntilie -Jerry/Ray c/AT (1ST WEEK ON NO.1)
2. Bado tunapanda – Tip Top connection (3 WEEKS ON NO.1)
3. Teja - Lady JD
4. Karibu tena - Johmakini
5. Salasala - Godzila
6. Nauza kura yangu - Bonta
7. Shoga-Shaa (3WEEKS ON NO.1)
8. Chembambament-Noorah/Ngweair
9. Demu wangu-Jaffaray/TID (2 WEEKS ON NO.1)
10. Iveta-Sajna
11. Unikimbie-Amini
12. Ngosha the swaga Don-Fid Q
13. Mtoto mtundu-Juma Nature
14. Mkono mmoja - Chege, Wahu,
Temba (3WEEKS ON NO.1)
15. Sina raha-Sam
16. Usije mjini-Mwana fa/AY
17. Kisiwa cha ma lovedavi – Z-Anto
18. Songa mbele-Alpha/AY
19. Tamaa mbaya – 20% (NEW)
20. Mechi za ugenini – Roma (NEW)


compiled by mc george/ijumaa

No comments: