
Ili kuwahakikishia wazazi wa Jennifer kuwa hatoathirika kimasomo pale atakapojiijngiza kwenye filamu, msanii Kanumba alisema kuwa iwapo Jennifer atashuka chini ya nafasi ya tano, atakuwa amepoteza nafasi ya uigizaji. Kitendo hicho kwa maana nyingine, kilikuwa kama kichochoe cha msanii huyo kufanya vizuri darasani, kwani alishika nafasi ya 2 katika mtihani wa muhula wake wa mwisho. Jennifer ni mwanafunzi wa Diamond Primary School, ya Upanga jijini Dar es salaam.
Sinema iliyomtambulisha mtoto huyu ni This Is It iliyotengenezwa na Kanumba Great Films na kufuatiwa na Uncle JJ, zote zikiwa zinafanya vizuri sokoni. Wiki iliyopita, Jennifer alipata tuzo ya msanii bora chipukizi iliyotolewa na tamasha la filamu zanzibar (Ziff) kutokana na uchezaji wake mzuri katika filamu ya This is It.
Kanumba ana stahili kuwa mfano wa kuigwa kwa maproducer wengine wanaochukua watoto wa watu na kuwaingiza kwenye sanaa. Suala la elimu lipewe kipaumbele na liwe moja ya masharti ya kumfanya mtoto kukubalika kuingia kwenye sanaa. kwa staili hii watoto wengi watanufaika bila kuathiri maendeleo yao ya kielimu.
No comments:
Post a Comment