Wednesday, August 10, 2011

SERIKALI YAHIMIZWA KUTETEA HAKI ZA WATOTO.

 
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Asha Rose Migiro akizungumzia umuhimu wa Taifa kusimamia haki ya mtoto ya kuishi kwa amani na furaha bila kufanyiwa Ukatilii wa aina yoyote katika Kilele cha uzinduzi wa ripoti ya Utafiti na Mpango wa Kitaifa wa kushughulikia "Ukatili kwa Watoto" na mpango wa Udhibiti wa Taifa.

Mabalozi wawakilishi wa nchi mbalimbali nchini wakifuatilia uzinduzi wa ripoti hiyo.
Watoto wa Shule mbalimbali za msingi wakiandamana katika sherehe za uzinduzi wa ripoti ya Utafiti na Mpango wa Kitaifa wa kushughulikia "Ukatili kwa Watoto" na mpango wa Udhibiti wa Taifa.
Katikati ni Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Umoja Mataifa Bi. Asha Rose Migiro,  wa pili kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba, wa kwanza kushoto Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa, wa Pili Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI (Elimu) Bw. Majaliwa Majaaliwa na wa Kwanza Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Haji Mponda kwa pamoja wakikaribishwa maandamano yaliyokuwa yakiingia katika viwanja vya Karimjee.
Wadau na watu mbalimbali kutoka taasisi za Kimataifa na  Kitaifa wakifuatilia kwa umakini kilele cha uzinduzi huo.
Dr. Rose akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi rasmi

No comments: