Sunday, September 25, 2011

MBIO ZA MBUZI ZILIVYOFANA JIJINI

 Ofisa Uhusiano wa Benki ya NBC, Eddie Mhina (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 1.8 kwa mshindi wa mbio za mbuzi za NBC Select Sprint ambazo mbuzi mwenye namba sita aliyepewa jina la ‘The Joisey Goatess’ alishinda. NBC ilikuwa mmoja wa wadhamni wa mbio za mbuzi za mwaka huu zilizofanyika katika viwanja vya The Green Barabara
ya Kenyatta, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Kutoka kushoto Meneja Uhusiano na habari za mtandao wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,Afisa Udhamini Ibrahim Kaude,Mkuu wa Udhamini  George Rwehumbiza wakifurahia  ushindi wa mbuzi waliomdhamini ‘Vodafasta’katika mbio za mbuzi zilizokuwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia vituo vya watoto yatima na wasiojiweza hapa nchini, mbio hizo zilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
 Mbuzi namba sita akimaliza mbio za mbuzi za  NBC Select Sprint
zilizodhaminiwa na benki ya NBC na kuibuka kidedea  wakati wa
mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi katika viwanja vya The Green, Barabara ya Kenyatta, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya mbuzi’Vodafasta’ waliodhaminiwa na Vodacom Tanzania wakishiriki mbio hizo zilizokuwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia vituo vya watoto yatima na wasiojiweza hapa nchini, mbio hizo zilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wapenzi wa mbio za mbuzi akipiga kinywaji chake kilainiiiii katika viwanja hivyo wakati mbio hizo zikiendelea zilizokuwa na  lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia vituo vya watoto yatima na wasiojiweza hapa nchini, mbio hizo zilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mbuzi wakishindana ili kumpata mshindi wa mbio za mbuzi za NBC Select Sprint zilizodhaminiwa na benki ya NBC wakati wa mashindano ya mwaka huu ya mbio za mbuzi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Wapenzi wa mbio za mbuzi wakifuatilia mbio hizo zilizodhaminiwa na Vodacom Tanzania hapo jana zilizo kuwa na  lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia vituo vya watoto yatima na wasiojiweza hapa nchini.
Mshereheshaji wa mbio za mbuzi zilizodhaminiwa na Vodacom Tanzania hapo jana akiingia kwa madaha.

No comments: