Wednesday, September 14, 2011

SWALA YA GHAIBU KWA WALIOFARIKI KUTOKANA NA AJALI YA KUZAMA KWA MELI ZANZIBAR

Kwa mashirikiano ya pamoja  ya wanafunzi wa Tanzania wanaosoma vyuo mbali mbali nchini Malaysia, kufuatia ajali ya kuzama kwa meli siku ya tarehe 10/9/2011 iliyosababisha vifo vya watu wanaofikia zaidi 240. Siku ya IJUMAA tarehe 16 Sept. 2011 patakuwa na swala ya ghaibu (Swala ya Maiti) itakayoswaliwa mara tuu baada ya swala ya Ijumaa kwenye msikiti mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kimataifa (International Isalmic University Malaysia)  campus ya Gombak. Swala hiyo itafuatiliwa na kisomo cha Qur'ani kwa ajili ya kuwaombea dua ndugu hao waliofariki. Tunaomba taarifa hii wafkishiwe wanafunzi wote wa Tanzania wanaosoma Malaysia.
 
Tunategemea mashirikiano makubwa katika mkusanyiko huu wenye nia ya kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja katika kuwaombea marehemu wote.

Kwa wale ambao hawajawahi kufika campus ya IIUM Gombak unaweza kupanda basi nambari 91 kutokaKOTA RAYA au shuka LRT Rapid KL kituo cha Gombak kisha chukua basi nambari 231 au ulizia kupitia nambari ya simu 0173416793.



Ahsante
Kwa niaba ya kamati ya muda ya maandalizi.
IIUM, Gombak

No comments: