MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MJINI MH. MOHAMMED DEWJI AMETOA PONGEZI
ZA DHATI KWA KOCHA WA SIKU NYINGI HAPA NCHINI CHARLES BONIFACE MKWASA KWA
KUCHAGULIWA KUWA KOCHA MKUU WA TIMU YA SOKA YA TAIFA ‘TAIFA STARS’.
MH.MBUNGE HUYO ALMAARUFU KAMA ‘ MO’ AMBAYE ANASIFIKA KWA KUHAMASISHA MICHEZO PIA
AMELISIFU SHIRIKISHIO LA MPIRA WA SOKA TANZANIA (TFF) KWA KUONYESHA UZALENDO KWA KUMCHAGUA
KOCHA WA HAPA NYUMBANI KUFUNDISHA TIMU YA TAIFA.
PONGEZI HIZO AMEZITOA KUFUATIA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA KATIBU
MKUU WA TFF BW. ANGETILE HOSIAH ALIYOITOA SIKU YA JUMAMOSI KWA VYOMBO VYA
HABARI KUWA MKWASA ALIYEKUWA AKIIFUNDISHA TIMU YA TAIFA YA SOKA YA WANAWAKE YA
TANZANIA ‘TWIGA STARS’ AMECHAGULIWA KUWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA
BARA.
KATIKA UTEUZI HUO KOCHA MACHACHARI ANAYEFUNDISHA TIMU YA
COASTAL UNION YA TANGA JAMHURI KIHWELO ‘JULIO’ AMETEULIWA KUWA KOCHA MSAIDIZI
WA TIMU YA TAIFA NA MCHEZAJI WA ZAMANI WA KLABU YA SIMBA KHALID ABEID AMECHAKUGULIWA
KUWA MENEJA MPYA WA TIMU HIYO WAKATI WA MICHUANO YA CECAFA ITAKAYOFANYIKA KATIKA
MIJI YA DAR ES SALAAM NA MWANZA KUANZIA NOVEMBA 25 HADI DISEMBA 10 MWAKA HUU.
KATIKA PONGEZI HIZO MH. ‘MO’ AMESEMA KWA HAKIKA TFF
IMEONYESHA UZALENDO NA KUMTAKIA MKWASA MAFANIKIO PINDI ATAKAPOANZA JUKUMU LA
KUONGOZA JAHAZI LA TIMU YA TAIFA.
AIDHA MH. ‘MO’ AMEITAKIA MAFANIKIO MEMA TIMU YA TAIFA IKIWA
CHINI YA KOCHA MKWASA HUKU AKISEMA ‘ MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI
TAIFA STARS, MUNGU MBARIKI MKWASA NA KAMATI NZIMA YA UFUNDI YA TIMU HIYO.
AKHSANTEN.
Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,
No comments:
Post a Comment