Tuesday, November 1, 2011

Vodacom yawekeza milioni 90 kwa shule 20 za msingi mkoa wa Dar es Salaam


Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi msaada wa madawati Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwongozo  Elly Shuma  kwa niaba ya walimu wenzake wa shule tano zilizonufaika na msaada huo wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni shirini na ishirini na tano elf(20,25,000)kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.
Pichani juu, Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwongozo iliyopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dares Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati  225 yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Milioni 20,25,000,kwa shule tano za wilaya ya Kinondoni na Ilala,Jumla ya  madawati Elf moja  yenye thamani ya Milion 90 yametolewa msaada kwa shule 20 za Mkoa wa Dares Salaam  mwaka huu.
Jana Vodacom Foundation imekamilisha kwa kutoa madawati 225 kwa shule 5 za Wilaya Ilala na Kinondoni ikiwa ni zoezi lililoanza mwezi wa nne la kutoa msaada wa madawati 1000 katika Mkoa wa Dar es salaam.

Tatizo la uhaba wa madawati katika shule mbalimbali za msingi hapa nchini ambalo limekuwa kwa namna moja ama nyingine likichangia kukosekana kwa mazingira dhabiti mashuleni linazidi kupata msukumo wa kutatuliwa kutoka kwa taasisi na mashirika binafsi nchini.

Moja ya mashirika hayo ni mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambao leo umekabidhi madawati mia mbili na ishirini na tano yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini na ishirini na tano elf,ikiwa ni utekelezaji wa muendelezo wa utoaji wa madawati katika shule za msingi za  mkoa wa Dar es salaam.

Akizungumzia mradi huo Afisa Mkuu wa masoko na uhusiano wa kampuni hiyo Bi. Mwamvita Makamba  amesema mradi huo ni sehemu ya kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wa kitanzania kama nyenzo muhimu ya kuwajengea mazingira bora ya kuja kujisaidia katika maisha yao na kulisadia pia taifa katika fani  mbalimbali.

Vodacom Foundation imekuwa ikiweka mkazo kusaidia sekta ya elimu kama eneo muhimu la kuchangia nguvu na juhudi za serikali katika ustawi wa jamii nchini, hii ni awamu ya pili kwa mwaka huu na ni imani ya Vodacom kwamba madawati hayo yatapunguza uhaba katika shule ambazo zitaguswa.

"Tunatambua ukubwa wa tatizo na kwamba lipo takribani nchi nzima na tunaguswa nalo kama kampuni yenye kujali maisha ya watanzania na ndio maana kila mwaka tumekuwa tukiendesha kampeni maalum ya kuchangia madawati ni imani yetu kwamba ipo siku changamoto hii itabakia kuwa historia"Aliongeza Mwamvita Amesema ukosefu wa madawati nchini ni changamoto ambayo dhahiri ahitaji kufumbiwa macho wala kuzibiwa masikio inahitaji nguvu za pamoja za kila wadau ili kuwawezesha wanafunzi ambao ndio nguvu kazi ijayo ya taifa kuwa na mazingira bora, salama na kuwawezesha kufanya vema katika masomo yao.

"Inaumiza sana unapoona watoto wameketi sakafuni au kubanana katika dawati moja darasani, hii lazima itapunguza uwezo wao wa uelewa na ufuatiliaji masomo darasani ndio maana tukaamua kama kampuni inayoungwa mkono na watanzania kuonesha upendo wetu kwa kuwa na kampeni kabambe ya kusaidia madawati mashuleni"Amesema Afisa Mkuu wa  Masoko na uhusiano wa Vodacom.

Awamu hii imenufaisha shule za msingi tano ambazo ni Maarifa shule ya Msingi (Ilala) Kombo shule ya Msingi (Ilala) Vingunguti Shule ya Msingi (Ilala) Mwongozo Shule ya Msingi (Kinondoni) Kimara B Shule ya Msingi (Kinondoni)

No comments: