Wednesday, December 7, 2011

CHAMA CHA MA MC WASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU

  
 ..SAA iko juu!!
...baadhi ya Ma MC wakifurahia muziki ulioimbwa na Makasy maalum kukipongeza chama cha Ma MC 
 ...wakisakata rhumba mpaka chini
 Mama Henjewele akimtunza Makasy wakati akitoa burudani
 Mzee Makasy akisalimiana na Mlezi wa SAA, Mzee Mdachi (kulia)
 Makassy Jr na mkewe wakisakata Rhumba
 Mzee Makassy na mwanae Makasy Jr wakiburudisha wagani waalikwa
 Kutoka kushoto: Mzee Isaya na mkewe Mariyon, mzee Laurian na Mkewe Angelina wakikata keki kwa pamoja kama ishara ya upendo
 Mzee Isaya Nzibukila akilisha keki mkewe Bi. Mariyon katika sherehe hiyo. Wazee hawa wako kwenye ndoa kwa muda wa miaka 53 sasa!
 Bi. Angelina Itumbaki akimlisha keki mumewe Laurian Itumbaki katika sherehe hiyo. Wazee hawa wako kwenye ndoa kwa muda wa miaka 52 sasa!
Baadhi ya viongozi wa Ma MC, wakiwa katika picha ya pamoja na wanandoa wazee.

Chama cha Washereheshaji wa sherehe mbalimbali nchini, Sherehe Arts Association (SAA) mwishoni mwa wiki iliyopita kilisherehekea sherehe za miaka 50 ya Uhuru kwa kuandaa hafla pamoja na wazee walioko kwenye ndoa kwa muda wa miaka 50 sasa. Sherehe hiyo, ambayo iliongozwa na MC mkongwe na Mlezi wa chama hicho, Mzee Mdachi, ilifanyika kwenye ukumbi wa Lamada Hotel iliyopo ILALA jijini Dar es salaam na kudhaminiwa na TBL kupitia kinywaji chake cha Konyagi.

No comments: