Tuesday, May 29, 2012

SPRITE HASHEEM THABEET U17 BASKETBALL CLINIC, JUNI 1-2, 2012


From Left TBF Asst. Sec. Gen. Michael Maluwe, Cocacola Asst. Brand Manager Warda Kimaro, TBF Vice President Magesa, Hasheem Thabeet and Cocacola PR/Media consultant Gerald.


Kwa niaba ya Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF), tuna furaha kutangaza kwamba Kampuni ya CocaCola imekubali kudhamini mafunzo maalumu (kliniki) ya mpira wa kikapu mwaka huu kwa ajili vijana wa chini ya miaka 17  wavulana na wasichana kutoka mikoa sita ya Tanzania.

Kliniki hii itaendeshwa na Mtanzania, Mchezaji nyota wa kikapu anayecheza ligi ya NBA  Hasheem Thabeet, wa timu ya Portland Trail blazers, nyota hyo tayari yupo nchini tayari kwa ajili ya kliniki hii kufanyika katika viwanja vya mpira wa kikapu Don Bosco, Upanga, Dar Es Salaam.

Mikoa ambayo itashiriki katika kliniki ya mwaka huu ni Mwanza, Mbeya, Dodoma,Kilimanjaro, Arusha, Unguja, Pemba na mkoa mwenyeji wa Dar es Saalaam.

Takribani vijana 200 watashiriki katika kliniki hii, Hasheem atakuwa akisaidiwa na makocha wa ndani 3 na 6 wachezaji wakubwa yumbani,  hivyo wote watanufaika kutokana na kliniki hii.

Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Kampuni ya CocaCola  kupitia kinywaji cha SPRITE kwa kudhamini tukio hili na tunaomba makampuni mengine yaige mfano wa Cocacola.

Pia tunamshukuru Hasheem Thabeet kwa kukubali kufanya kliniki hii kama sehemu ya wajibu wake wa kijamii, kwa hili anastahili pongezi za dhati kwa kuwa na moyo wa kizalendo na kuweka mbele maslahi ya Taifa  na jamii yake na wanamichezo wengine wakubwa ni vizuri wakaiga mfano wake.

Tunawashukuru CocaCola kwa msaada wao katika matukio yetu mengi wao wamekuwa wakitusaidia katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje na kliniki za vijana, na wamekuwa wakifanyia marekebisho viwanja vyetu vya mpira wa kikapu baadhi viko katika miji ya Dar es Salaam, Pwani, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Arusha na Kilimanjaro .

Tunaiomba CocaCola na taasisi nyingine kuendelea kutusaidia katika matukio yetu yajayo mwaka huu kama kliniki nyingine itakayofanyika Arusha tarehe 9-10 Juni itakayoendeshwa na kocha wa NBA toka Marekeni, taarifa zaidi zitatolewa baadae, kombe laTaifa  mwezi Oktoba na Mashindano ya Mataifa ya FIBA kanda ya 5  yanayotarajiwa kufanyika hapa jijini Dar es Salaam Desemba, 2012.

Pia tunaiomba CocaCola kuendelea na ukarabati wa viwanja zaidi nchi nzima kwa faida ya vijana wetu, hii inaendana na mpango mkakati wetu wa uendelezaji wa miundombinu ya michezo.

Nawashukuru sana,

Phares Magesa
TBF- Vice President

No comments: