Monday, June 11, 2012

BURUDANI ZA WATOTO NDANI YA DAR LIVE

Keki ya bethidei inayotolewa na uongozi wa Dar Live kila Jumapili kwa watoto wanaosherehekea siku yao ya kuzaliwa kwa siku hiyo.
 
Mmoja wa watoto husika na bethidei (kulia) akijitayarisha kukata keki.
 
…Akimlisha keki MC wa watoto wa Dar Live.
 
Mtoto mwingine akisherehekea bethidei yake kwa kumlisha keki mama yake.
 
Watoto wakifurahia michezo iliyokuwa ikifanywa na ngongoti na ‘sungura’.
 
Ngongoti wakiwa kazini kuonyesha umahiri wao wa kutoa burudani kwa watoto.
 
Mmoja wa ngogoti akiwa amembeba mtoto katika kuongeza ladha ya burudani hiyo.
 
Watoto wakifurahia onyesho lililotolewa na ‘kinyago’.
 
Moja ya burudani ambazo zilivutia hisia za watoto hadi wakabaki kushangaa.
 
Ndege ya Dar Live ni moja ya vivutio vikubwa kwa watoto siku ya Jumapili.
 
Mchezo wa bata wenye kuzunguka ni moja ya burudani kabambe za Dar Live siku ya Jumapili kwa watoto.
 
Disko la watoto la kwenye maji huwarusha roho watoto kwa hisia za furaha kubwa.
 
…Disko la kwenye maji likiwa limepamba moto.
KAMA kawaida siku ya Jumapili jana ilikuwa na mvuto mkubwa kwa wapenzi wa burudani ambao hufika kwenye ukumbi wa maraha wa Dar Live huko Mbagala jijini Dar es Salaam. Jumapili huvuta makundi makubwa ya watu kwani huwa ni siku inayojumuisha burudani ya watoto ambao pamoja na michezo mbalimbali huwa kuna kivutio cha keki maalum ambayo hutolewa na uongozi wa kituo hicho kwa ajili ya watoto wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa (bethidei). Keki hiyo hutolewa bure kwa watoto husika.
Vilevile, michezo mingi zaidi imebuniwa na kuboreshwa zaidi kwa ajili ya kuwafurahisha watoto ambao hufika hapo kufurahia siku na jamaa zao. Ni kituo cha maraha zaidi nchini ambako watoto wanaweza kufaidi siku ya wikiendi na familia zao tena kwa bei nafuu.

No comments: