Tuesday, June 12, 2012

'Wazee Wa Kazi' Serengeti Freighters And Fowarders Kusafisirisha BURE Mizigo Ya Misaada Kwenda Kijijini Mahango, Tanzania!

 Ni baada ya kutambua mchango mkubwa uliofanywa na Bi Karrima Carter na mwanawe Lukeman Carter wa Norrwich, Uingereza. Mtoto Luke baada ya kuona picha za wanafunzi wa kijijini Mahango kwenye Mjengwablog aliamua kutumia kazi ya project ya shuleni kwake kukusanya pesa kwa malengo zifikie shilingi milioni moja za Kitanzania ili ziende kijijini Mahango kusaidia kukarabati darasa la wanafunzi na chumba cha maktaba ya wanafunzi pia. Mwitikio ukawa mkubwa kuliko alivyotarajia Luke na wengine. Zikawa zaidi ya shilingi milioni moja na maboksi zaidi ya 35 ya vifaa vya shule ikiwamo vifaa vya michezo pia.

Na hapa nyumbani Tanzania kuna wengi wengine waliomuunga mkono Lukeman Carter. Kupitia Mjengwa blog zimechangwa takribani shilingi milioni nne.

Na kusafirisha maboksi hayo ya misaada iliyokusanywa na Lukeman na Bi Karrima Carter kufika Tanzania ingekuwa ni gharama kubwa sana. Lakini, Mtanzania, mzalendo Chris Lukosi na wenzake wa Serengeti Freighters And Forwarders ama maarufu kama ' Wazee Wa Kazi' jana wamepokea mizigo hiyo kutoka kwa Bi Karrima Carter na wamejitolea kusafirisha bure mizigo hiyo ya misaada! Huo ni uzalendo uliokidhi viwango. Msaada huu utasaidia kubadilisha maisha ya wengi Mahango na vijiji vya jirani kule Madibira, Mbarali Mbeya. TUNAWASHUKURU SANA!


Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.com

No comments: